Quantcast
Channel: Global Voices in Swahili » Habari za Hivi Punde
Viewing all 93 articles
Browse latest View live

Misri Yawahukumu Kifo Wafuasi 529 wa Muslim Brotherhood

$
0
0
A state-of-the-art execution machine designed by @Ternz to help Egypt execute 529 Muslim Brotherhood supporters

Mashine maalumu ya kunyongea iliyobuniwa na @Ternz kuisaidia Misri kuwanyonga wafuasi 529 wa Muslim Brotherhood

Leo, [tarehe 24 Machi] imewahukumu kifo wafuasi 529 wa chama cha Muslim Brotherhood kwa kuhusika na vitendo vya ghasia huko Minya, kaskazini mwa Misri, mwezi Agosti mwaka jana.

Ghasia hizo zililipuka kufuatia kung'olewa madarakani kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Mohammed Morsi, ambaye alikuwa kiogozi wa kundi hilo la Muslim Brotherhood leader, na kusababisha mamia ya wafuasi huo kupoteza maisha yao.

Ghasia za Minyah zilisababisha kufa kwa afisa mmoja wa polisi – kosa la jinai ambalo ndilo lililosababisha kushitakiwa kwa washikiwa wote.

Nchini Misri, hukumu hiyo, moja ya hukumu kubwa kabisa ya kifo kuwahi kutolewa katika historia ya leo, ililaaniwa au kuungwa mkono, kutegemeana na mtazamo wa kisiasa wa aliyetoa maoni. Mada Masr alikuwa na orodha ya miitikio hapa.

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anasema hukumu hii, ambayo hukumu ya mwisho kabisa inategemewa kusomwa tarehe 28 Aprili, imevunja rekodi mpya ya dunia.

Mwanablogu huyo anaeleza:

Tunayo idadi kubwa ya wagonjwa wa kansa ya damu [Hepatitis C] duniani, tuna idadi kubw aya udhalilishaji wa kijinsia duniani na leo tumevunja rekodi kwa kuwa na hukumu ya kifo kwa watu wengi kwa mpigo kuwahi kutolewa mahakamani katika kesi moja!!! Ninazungumzia kuhusu hukumu ya kihistoria ya mahakama iliyotolewa na mahakama ya jinai ya Minya dhidi ya washitakiwa 529, ndio ile ambayo duniani yote inaizungumzia.

Zeinobia anaongeza:

Nitazungumzia ukweli usiohitaji mjadala hapa :

washitakiwa 529 wamehukumiwa kifo na wengine 15 wakionekana hawana hatia kufuatia kesi ya Minya.
Wengine 139 walishikiliwa kwenye kesi hiyo wakati waliobaki ama waliachiwa kwa dhamana au kwa utaratibu.
Washitakiwa 51 walihudhuria mashitaka hayo mahakamani kwa sababu hapakuwa na sehemu ya kuwawezesha wote kusimama mahakamani kwa wakati mmoja.
Mashitaka hayo yalianza siku ya Jumamosi na kukamilika siku ya Jumatatu.
Wanasheria wa washitakiwa waliomba kubadilishiwa jaji lakini ombi lao lilitupiliwa mbali.
Wanasheria waliokuwa wanawatetea “washitakiwa wasiokuwepo” hawakuruhusiwa kuwatetea washitakiwa !!!
Washitakiwa 529 wametuhumiwa kuwaua msaidizi wa kituo cha polisi cha Matay Sheriff Mostafa El Attar!!
Hii ndio hukumu kubwa zaidi kwa watu wengi kuwahi kutolewa kwa wakati mmoja katika historia ya mahakama za Misri.

Mwandishi wa Misri Bel Trew anashangaa:

Siwezi kufikiri itakavyokuwa wakati wa kuwanyonga watu 529. Kama ilichukua dakika 5 tu kumnyonga mtu mmoja kwa maana hiyo yatahitajika masaa 44 mfululisho kuwanyonga hawa jamaa

Na Mmisri @Ternz, anayekubali kuwa ndio kwanza kaanza kuchora katuni wiki mbili zilizopita, amekuja na suluhisho: Mashine ya kisasa ya kunyongea.

Anaeleza[ar]:

Wakati nikiwa nimepumzisha akili, nikajiuliza: Ninawezaje kulitumikia taifa langu vyema? Ninawezaje kuliletea faida taifa langu na kulisaidia? Kwa hiyo nikachukua kalau na kubuni mashine ambayo Misri inaihitaji wakati huu

Na hapa unaweza kuona ubunifu wake:

Kama mchango wangu kwa taifa langu katika kufanikisha hukumu ya kifo kwa ufanisi, ninatumaini kuwa kifaa hiki kitawavutia maafisa. Hii ni mashine ya kisasa ya kunyongea

Wakati huo huo, mwandishi anayeishi Uingereza, Inigo Gilmore anahitimisha:

Misri inataka watalii warudi, wakati inawabana waandishi mithili ya wanyama; inahukumu mamia ya watu kifo kwa mashitaka bandia?


Mlipuko wa Homa ya Ebola Waua Watu 59 Nchini Guinea

$
0
0
Ebola virus virion via wikimedia Commons -  Public Health Image Library, #10816- public domain

Virusi vinavyosababisha Ebola viitwavyo virion kupitia wikimedia Commons – Picha ya Maktaba ya Afya ya Umma, #10816- kwa matumizi ya umma

Mlipuko wa homa ya Ebola umeua watu wasiopungua 59 nchini Guinea na matukio kadhaa yanayohofiwa kuwa ya homa hiyo yamekaribia kwenye mjini mkuu Conakry hiyo ikimaanisha kuwa ugonjwa huo unaweza kuenea kwenye mji mkuu wa Guinea. Barbara Krief anatoa taarifa za hivi karibuni [fr]:

Au moins huit agents de santé ont été tués à ce jour. En collaboration avec le ministère guinéen de la Santé, l'Unicef a rapidement livré dans les zones les plus affectées cinq tonnes de médicaments et d'équipements médicaux tels que des gants, nattes plastiques, couvertures, protège-nez, et des solutions de réhydratation orale et intraveineuse pour protéger le personnel médical et traiter les malades

Kadri ya wafanya kazi wa afya nane wamepoteza maisha mpaka sasa. Kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Guinea, UNICEF imepeleka tani tano za madawa na vifaa vya matibabu kama vile glovu za mikononi, vitambaa, mablanketi, vitambaa vya kufunika uso, na maji ya kupunguza upungufu wa maji mwilini kuwalinda wafanyakazi wa afya na kuwatibu wagonjwa.

Hapa kuna video yenye taarifa za namna ya kujilinda na virusi vya Ebola :

Tetemeko Kubwa Laitikisa Chile Kaskazini, Lafuatiwa na Tahadhari ya Tsunami

$
0
0

Tetemeko kubwa lenye vipimo vya tetemeko 8.2 limeikumba Chile kaskazini majira ya saa 2:46 usiku na kusababisha tsunami aliyosababisha wasiwasi nchini humo kama video ifuatayo inavyoonyesha:

Kiini cha tetemeko hilo kilikuwa takribani kilometa 89 kusini mashariki mwa Cuya, mbele kidogo ya pwani ya Tarapaca.

Ramani: Kiini cha tetemeko hilo la ukubwa wa 8.2 kaskazini mwa Chile

Serikali iliwaomba wananchi kuondoka eneo lote la pwani kufuatia mawimbi ya kwanza ya bahari yalifika eneo la Iquique.

Katika mkusanyiko huu wa habari katika tovuti ya Nacion.cl, kuna picha kadhaa za watu wakielekea kwenye maeneo ya vilima na madhara ya kiwango fulani yalisababishwa na tetemeko hilo. 

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twita walisambaza taarifa za muhimu, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Taifa ya Mambo ya Dharura (ONEMI):

Wakati wa tishio la Tsunami, endoka kwa mguu nenda kwenye eneo la karibu zaidi kukutania.

Usisahau mbwa wako, ni lazima waondoke kwa dharura pamoja nawe. Tafadhali chukua tahadahri ya #Tsunami #Terremoto [tetemeko] #Iquique #Arica

Wengine walitoa maoni yao kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali wakilinganisha na tetemeko kubwa lililowahi kutokea mwaka 2010:

Wamejifunza kwa makosa waliowahi kuyafanya: wametoa tahadhari ya kutokea tsunami, na kushauri watu kuondoka maeneo yenye hatari na tayari jeshi liko mtaani. Mwisho, wamejiandaa.

Habari zinazoendelea

Tetemeko Kubwa Lizitikisa Chile na Peru

$
0
0
Sismo

Picha imechukuliwa kutoka kwa mtumiaji wa Twita @24HorasTVN

[Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa za intaneti za lugha ya Kihispania isipokuwa ikielezwa vinginevyo.]

Tetemeko  kubwa lenye vipimo vya tetemeko 8.3 limeitikisa sehemu ya kaskazini mwa Chile na Kusini mwa Peru, pamoja na maeneo ya jirani nchini Bolivia, saa za jioni siku ya Jumanne ya April mosi, 2014, hali iliyosababisha tishio la tsunami kwenye ukanda huo wa pwani.

Watu sita wameripotiwa kupoteza maisha nchini Chile, ikiwa ni pamoja na mwanamme mmoja raia wa Peru. Nchini Peru, hakuna taarifa za madhara makubwa katika majiji matatu ambapo nguvu ya tetemeko hilo ilikuwa kubwa zaidi – Tacna, Moquegua na Arequipa.

Raia wa Peru waliingia kwenye mtandao wa Twita wakati na baada ya tetemeko hilo. Ilisemekana kuwa kwenye jiji la Tacna hapakuwa na umeme kufuatia kuangua kwa nguzo za umeme:

Kwenye jiji la Tacna, mtikisiko ulikuwa mkubwa, jiji halina umeme.

Taarifa kutoka kwenye kituo cha Radio cha La Linterna kilitoa taarifa za kina zaidi:

Taarifa kutoka Tacna zinasema kuna tetemeko kubwa limetokea huko sekunde kadhaa zilizopita.

Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zinatangazwa, hapakuwa na umeme wala huduma ya mawasiliano ya simu za mkononi mjini Moquegua:

Maeneo ya Tacna na Moquegua hayana umeme. huduma za makampuni ya simu ya Movistar na Claro hazipatikani baada ya tetemeko…

Kutoka Chile zilikuja ripoti za watu kutakiwa kuhama makazi kwenye maeneo ya ukanda wa pwani ya kaskazini kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa tsunami:

HABARI MPYA – Zoezi la kuwahamisha watu kaskazini mwa Chile lilifanyika kwa utulivu, kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyeko Arica.

PICHA: Hivi ndivyo sehemu za pwani ya Chile zinavyohamwa kufuatia tishio la tsunami.

Hali kadhalika, kulikuwa na amri ya kuhama makazi nchini Peru  baadhi ya majiji kusini mwa nchi hiyo:

DHARURA: Amri ya kuhama makazi kwenye pwani ya Peru: Arequipa, Ica, Tacna.

DHARURA – TETEMEKO NCHINI CHILE: Mamlaka za Peru zimeliambia shirika la habari la AFP kuwa zinawahamisha watu kwenye eneo la kusini la nchi hiyo.

DHARURA – TETEMEKO NCHINI CHILE: Njia zote kuelekea [pwani ya Lima] Costa Verde kutoka [wilaya za] San Miguel, Magdalena, San Isidro, Miraflores na Barranco jijini Lima.

Mawimbi ya kwanza ya tsunami yaliripotiwa kuonekana kwenye pwani za Ilo na Tacna kusini ya Peru:

Mawimbi ya Tsunami yaliwasili La Punta Callao saa 2:31 jioni., Ica saa 1:39, Tacna na kwa mji wa Moquegua hayo ndiyo yanawasili.

Wakati huo huo nchini Chile, kuna taarifa za mitikisiko midogo baada ya tetemeko:

CHILE: Mitikisiko isiyopungua mitano ilitokea baada ya tetemeko hilo kubwa. Hizi ni nchi zenye hatari ya kukubwa na tsunami.

Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba

$
0
0

Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo.

Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? Wengine wana mashaka gatua hiyo inaweza kusababisha hali ya kutokuaminiana na kufuatiliwa kwa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii katika nchi zao.

Majadiliano ya kina na: Sana Saleem, Ivan Sigal na Solana Larsen.

Jijini Havana Unapata Kitabu Bure, Bila Malipo

$
0
0
Suelta masiva de libros en La Habana (Foto: Fernando Medina)

Utoaji wa vitabu kwa makundi nchini Havana (Picha na Fernando Medina)

Mamia ya watu walikusanyika kwenye bustani ya jiji la Havana, makao makuu ya Cuba, JUmapili iliyopita kushiriki kwenye zoezi la ugawaji wa vitabu. Mradi huo, uliongozwa na mwanablogu [es] na mwandishi wa Global Voices  Rafael González [es], ulikusudia [es] kuviacha vitabu mahali kokote kwenye bustani hiyo vikiwa na maelezo kwenye ukurasa wa kwanza yanayosomeka: “Kitabu hiki kinamilikiwa na yeyote atakayekipata na kukigawa kifurahiwe na wengine baada ya yeye kukisoma.”

Mradi halisi, ulianza kwenye mtandao wa Facebook [es], na kuchukuliwa na González, aliyewasiliana na waanzilishaji. Lu Di Piertro alitoa maoni kuhusu mradi huo: 

La idea no es nuestra, ya existe desde hace un tiempo y no sé exactamente quién la empezó. Un amigo, Rodri, que está también de organizador de este evento pensó en armar una suelta masiva y me propuso que hiciéramos este evento y gratamente fue muy aceptado. Nos parece bueno (el evento) por muchas razones (…): lo importante de leer, lo hermoso de dar, lo emocionante de soltar y la incertidumbre de no saber y confiar; fomentar la solidaridad y el espíritu del compartir social y culturalmente, abrir el corazón y atravesar fronteras. 

Wazo hili si letu, limekuwepo kwa muda sasa na sijui nani hasa alilianzisha. Rafiki yangu, Rodri, ambaye pia ni mwandaaji wa tukio hili alifikiri kutoa vitabu hivi vingi na kupendekeza kwangu kuwa tufanye tukio hili na kwa kweli limekubalika sana. (Tukio hili) linaonekana kuwa jema kwetu kwa sababu nyingi (…): Umuhimu wa kusoma, uzuri wa kutoa, furaha ya kuachia ulicho nacho na kutokuwa na uhakika wa kujua na kuamini; kuhamasisha ushirikiano na moyo wa kushirikiana kijamii na kiutamaduni, kufungua moyo wako na kuvuka mipaka.  

Wakati huo huo, mwandaaji mwingine, Rodri Bristot, added:

En lo personal, lo que me impulsa a organizar este evento de Suelta Masiva, tiene que ver con una idea un poco romántica: creo que hay cosas en la vida que debieran ser gratis, como la educación y la lectura; los libros no debieran ser solo para quienes pueden pagarlos, si no que deberían ser más accesibles, que la gente los encuentre en los espacios públicos sin tener que resignar algo (dinero o trabajo) para adquirirlos.

Kibinafsi, kilichonihamasisha kuandaa tukio hili la kugawa vitabu, ni wazo ambalo lina mvuto: Ninaamini kuwa kuna vitu kwenye maisha ambavyo vyapaswa kuwa bure, kama elimu na kusoma: vitabu havipaswi kuwa kwa ajili ya wale wanaovilipia pekee, vyapaswa kupatikana zaidi, watu walipate kwenye maeneo ya umma bila kuvilipia (iwe fedha au kazi) ili kuvipata.

Varios marcadores fueron compartidos en la cita (Foto: Fernando Medina)

Alama kadhaa za vitabu zilitumika wakati wa tukio(Picha na Fernando Medina)

Asubuhi ya Jumapili, Aprili 6, González akiwana na kikundi cha vijana 50, wakubwa kwa wadogo, aligawa vitabu kwenye Bustani yaH y 21, iliyopo El Vedado, Havana. Watu walitafuta kwenye mabenchi ya bustani hiyo, kwenye mizunguko ya katikati ya bustani na kati kati ya mizizi ya miti, na hata kuwafuata watu waliokuwa wanakuja bustanini hapo ili kupata vitabu hivyo. 

Mwandishi wa Cuba Dazra Novak alielezea uzoefu huo [es] kupitia blogu yake  [es]: 

He soltado cuatro libros hoy -con el mes, el año y la ciudad anotados en la primera página-, espero que los beneficiados la pasen tan bien como yo al leer dos de esos títulos, tan bien como la pasé al escribir los otros dos. No sé por qué sospecho que en algún momento volverán a mí para que yo pueda enrumbarlos de nuevo. Ahora que lo pienso, hoy –mañana, siempre- todos deberían hacer lo mismo.

Niligawa vitabu vinne leo -vikiwa vimeandikwa mwezi, mwaka na mji kwenye ukurasa wa kwanza -, ninaamini kuwa watakaovipokea watavifurahia kama nilivyovifurahia mimi wakati navisoma viwili kati ya hivyo, na kama nilivyoviandika viwili kati ya hivyo. Sijui ni kwa nini nina mashaka kuwa kwa wakati fulani vinaweza kunirudia ili na mimi nivitoe kwa mara nyingine. Sasa ninapofikiri tukio hilo, leo -kesho, na siku zote -kila mmoja afanye hivyo hivyo.  

*Picha kuu imepigwa na Fernando Medina.

Mgogoro Usiopewa Uzito Stahiki Nchini Burundi

$
0
0

Wakati nchi jirani ya Rwanda inagonga vichwa vya habari na maadhimisho ya mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 na kuongezeka kwa mvutano na Ufaransa, Burundi imeharibiwa katika kupuuzwa kwa mgogoro wa kisiasa na dalili za vurugu zinazoweza kusababisha mapigano mapya ya Wahutu na Watutsi. Tshitenge Lubabu nchini Burundi anatoa maoni kwamba mzizi hasa wa mgogoro ni viongozi wa sasa wa kisiasa:

 La plupart de nos dirigeants, bien ou mal élus, malgré de longues années de pouvoir, se sont illustrés par leur impéritie [..] Tous les mensonges sont bons pour confisquer le pouvoir. Quand leurs mandats, limités par la Constitution, arrivent à terme, des courtisans zélés, jamais repus, les supplient de ne pas partir. Comme si, sans eux, le soleil risquait de ne plus apparaître 

Wengi wa viongozi wetu, waliochaguliwa vyema au sivyo, licha ya kukaa muda mrefu madarakani, ni wazembe [..] uongo wowote ni mzuri kumfanya akwae madaraka. Wakati majukumu yao yanafikia mwisho kama ilivyoainishwa katika Katiba, wasaidizi wao wenye bidii, wasioridhika kamwe, huwaomba wasiachie madaraka. Ni kama wanafikiri bila wao, jua halitawaka kesho.

Niger Yapata Kituo Chake cha Kwanza cha Reli Baada ya Kusubiri kwa Miaka 80

$
0
0

Aprili 7, Niger ilizindua katika mji mkuu wa Niamey kituo chake cha kwanza cha treni kuwahi  [fr]. Mamlaka tayari ilikuwa na makadirio ya ujenzi wa kituo cha treni miaka 80 iliyopita lakini mradi kamwe haukuanzishwa. Tukio hilo litaanzisha ujenzi wa reli kati ya Niger, Benin, Burkina Faso na Côte d'Ivoire. Mtumiaji Twita Tanoussou katika Niamey aliweka picha kwenye mtandao ya kituo hicho cha reli:

 

Photos postsVideo posts


Chanzo cha Maji nchini China Chawekwa Kemikali Inayosababisha Kansa

$
0
0

Mamlaka ya jiji la Lanzhou imetoa angalizo kwa raia wake la kutokutumia maji ya bomba kutokana na maji hayo kugundulika kuchanganyikana na kemikali hatari, hali iliyopelekea maji ya viwandani kugombaniwa katika maduka mbali mbali ya jiji.

Kwa mujibu wa mamlaka ya jiji, kiasi kikubwa cha benzini, kemikali inayosababisha kansa, kimegunduliwa kwenye chanzo cha maji cha jiji hili. Wakati fulani, kiwango cha benzene kwenye maji ya bomba kilipanda hadi mara 20 ambacho ni kiwango hatari kabisa kwa matumizi. 

Lanzhou, jiji la viwanda lililopo Kaskazini Magharibi mwa China, linategemea sana mto wa njano kama chanzo chake cha maji. Miaka ya hivi karibuni, jiji hili lenye wakazi takribani milioni nne limeanza kuona matumaini ya ongezeko la uwekezaji wakati ambao taifa limebuni njia mpya za kuinua uchumi wa kanda masikini za magharibi. 

lanzhou

Wakazi wa Lanzhou wakigombania maji ya chupa mara baada ya mamlaka ya jiji kutoa tangazo la kutokutumia maji ya bomba. Picha kwa idhini ya mtumiaji wa Sina Weibo, Wangyangyagn de Xiaopengyou.

Kampuni ya Kifaransa ya utibuji wa maji, ijulikanayo kama Veolia, na wasambazaji wakuu wa maji jijini Lanzhou, ililiambia  shirika la habari la serikali la Xinhua kuwa, benzini iliyopo kwenye maji imetoka kwenye viwanda vya uchimbaji na usafishaji wa mafuta ya asili. 

Ofisi inayohusika na utoaji wa taarifa katika jimbo la Gansu, ambapo Lanzhou ikiwa ndio mji mkuu, iliweka ujumbe huu kwenye ukurasa wake rasmi wa sina Weibo ufananao na wa twitter: 

【未来24小时兰州居民不宜饮用自来水】4月11日凌晨3时起,兰州威立雅水务公司向水厂沉淀池投加活性炭,吸附有机物降解苯对水体的污染。11日上午11时,停运北线自流沟,排空受到污染的自来水。在此期间,市区降压供水,高坪及边远地区停水,限制生产性用水。未来24小时自来水不宜饮用,其他生活用水不受影响。

Kwa muda wa masaa 24 yajayo kuanzia sasa, maji ya bomba hatafaa kwa matumizi kwa wakazi wa Lanzhou. Kuanzia saa 9 usiku, Aprili 19, Lanzhou Veolia imeshaweka kemikali ya kaboni kwenye mapipa ya kampuni kwa lengo la kufyonza dutu za kioganiki kama namna ya kuyeyusha benzini iliyo kwenye maji hayo. Majira ya saa 5 asubuhi, April 11, kampuni hii ilisitisha utoaji wa huduma katika mfumo wa mabomba wa Kaskazini kwa lengo la kuyaondoa maji yaliyochanganyikana na kiasi kikubwa cha benzene. Katika kipindi hiki, kwa maeneo ya mijini, maji yatakuwa yakitolewa kupitia mbinu ya kupunguza kani eneo, lakini hakutakuwa na maji kwa mtaa wa Gaoping na maeneo mengine ya pembezoni. Utumiaji wa maji viwandani utazuiwa. Kwa kipindi cha masaa 24 yajayo, maji yanayotiririka hayatafaaa kwa matumizi ya kunywa, aina nyingine za maji hayatakuwa na shida.

Vyombo vya habari vya China vimeripoti kuwa, mwezi uliopita, wakazi wa Lanzhou walitoa malalamiko yao kuhusu harufu mbaya ya maji ya bomba, lakini viongozi wa jiji walisema kuwa ubora wa maji ulikuwa wa kiwango kilichokubalika. Raia kadhaa waliokuwa wakitoa taarifa za maji kuchanganyikana na kemikali hatari kwa kipindi hicho walijulikana kama “wavujisha tetesi” na “kushughulikiwa” kwa mujibu wa sheria. 

Tatizo la maji la Lanzhou limezidi kuchochea zaidi tatizo lisilozuilika la uchafuzi lililolishitusha taifa kipindi ambacho uanaharakati wa mazingira unaanza kushika kasi nchini China. Mwaka 2013,  mwanablogu mashuhuri na mwandishi wa habari wa zamani alianzisha  kampeni ya mtandaoni ya kuwataka watumiaji wa mtandao kupiga picha za uchafuzi wa mito katika maeneo wanayoishi.   

Uchavuzi wa maji kwa kemikali hatari huko Lanzhou imekuwa ni moja ya mada tatu zilizopewa kipau mbele katika mtandao wa Weibo siku ya Ijumaa usiku. 

Jarida la habari za Beijing liliweka taarifa hii kwenye ukurasa wake rasmi wa Weibo: 

【已切断污染源 政府免费提供安全水】兰州市应急处置领导小组基本找准了污染点,并马上予以切断。有关方面正从周边地区调运桶装水和瓶装水,将通过各区政府和辖区街道、社区,向广大市民免费提供

【Chanzo cha uchafuzi kimeshasitishwa. Serikali itaanza kutoa maji bure na yaliyo salama】. Jopo la dharura la Jiji la Lanzhou limeshafahamu chanzo cha uchafuzi wa maji na ilishatoa tamko la kukisitisha. Idara husika zimeshakusanya maji ya kwenye chupa na ndoo za maji kutoka katika maeneo ya jirani, na maji haya yatagawanywa kwa raia kupitia idara na jumuia mbalimbali..

Watumiaji wa Weibo wameikosoa serikali kwa kuruhusu kampuni isiyo milikiwa na wachina kusimamia mifumo ya maji ya jiji. Msanii wa uchekeshaji, Zhang Gang alitoa malalamiko yake:

 呼吁兰州政府调拨安全的饮用水,向市民免费发放!给出正面、准确的解释!接连不断的水污染让百姓情何以堪?洋鬼子控股的自来水厂能相信吗?把自来水厂卖给法国人,谁卖的?谁同意的?

Ninaiomba serikali ya Lanzhou ikusanye maji salama ya kunywa na iyagawe bure kwa raia wake!Yapaswa kutolewa jibu fasaha na la wazi!Ni udhalilishaji wa namna gani tatizo la uchafuzi wa maji liendelee kwa watu walewale. Tunaweza kuwa na imani na makampuni yanayosambaza maji yanayomilikiwa na wageni? Ni nani aliyeamua kuwauzia Wafaransa kampuni ya usambazaji wa maji, Ni nani alifanya hivyo?, na ni nani aliyetia saini?

Beijing Chuzi, mtumiaji wa Weibo aliye na marafiki zaidi ya nusu milioni, aliandika

这是政府做的最傻逼的一件事。最应该国营的放给外人做。我能不怀疑有人从中赚大钱么

Serikali imefanya jambo la kipumbavu kabisa. Imetoa [mamlaka ya usambazaji maji] kwa wageni wakati kimsingi mamlaka ilipaswa kuongozwa na serikali yenyewe. Nina wasiwasi kuwa mkakati huu umekuwa ni wa maslahi binafsi.

Serikali Mpya ya Waziri Mkuu Roger Kolo Yatangazwa Nchini Madagaska

$
0
0

Mtandao wa Tananews nchini Madagascar umechapisha orodha kamili ya mawaziri 31 wa serikali mpya ya Madagaska [fr]. Mitsangana Madagascar anasema kwamba orodha hiyo ina wanawake 6 na kuwa mawaziri 7 walikuwa kwenye baraza[fr] la serikali iliyopita ya mpito. Waziri mkuu wa zamani Beriziky aliitakia serikali kila la heri kwenye mtandao wa Twita:

Namuwasilisha Roger Kolo (@kolo_roger) kama waziri mkuu mpya. Shukrani nyingi kwa Malagasies wote #Madagascar

Watu 28 Wafariki, 268 Bado Hawajulikani Walipo Baada ya Feri ya Korea Kusini Kuzama

$
0
0

Feri ya Korea Kusini iliyokuwa inaelekea kwenye kisiwa cha mapumziko ilizama mnamo Aprili 16, 2014 na mamia ya abiria, ikiwa ni pamoja na wanafunzi 325 wa shule ya sekondari waliokuwemo. Zimetimia siku mbili tangu ajali hiyo itokee na watu 28 wamethibitika kufariki kufikia Aprili 18 na watu 268 bado hawajulikani walipo. Uwezekano wa kupona ni mdogo mno.

Picha tatu hapa chini zimetolewa hadharani kupitia ukurasa wa Facebook wa Coast Guard [ko]. Picha ya kwanza inaonyesha nahodha wa mashua akiwa miongoni mwa kundi la kwanza kuokolewa.

Image of the rescue operation, Image shared by Korean Coast Guard

Picha imetolewa kwa umma na Ukurasa wa Facebook wa Coast Guard wa Korea Kusini

Image of Sewol ferry rescue operation, Image shared by Korean Coast Guard

Picha ya Feri ya Sewol katika operesheni ya uokoaji, picha kwa hisani ya Ukurasa wa Facebook wa Coast Guard wa Korea Kusini

Image of Rescue Operation, Image shared by Korean Coast Guard's Facebook page

Picha ya operesheni ya uokoaji, kwa hisani ya Ukurasa wa Facebook wa Coast Guard wa Korea Kusini

Mijadala ya mtandaoni nchini Korea Kusini imefurika salamu za rambirambi kwa waathirika na wapendwa wao pamoja na hasira kali dhidi ya nahodha na wafanyakazi ambao waliokolewa mapema zaidi kabla ya abiria. Kilichochochea hasira zaidi ni tangazo linalosemekana kutolewa kwenye feri hiyo kuwaambia abiria waendelee kubaki ndani [ko], hata wakati feri ilipoanza kuzama.

Mwaka 2003 wakati wa maafa ya moto ya reli ya chini ya ardhi ya Daegu, idadi kubwa ya abiria walikufa wakati kondakta wa treni alikimbia baada ya kukwanyua ufunguo. Mimi nasikia masimulizi kuwa nahodha wa feri ya Sewol na kondakta waliokolewa mapema. Ningependa iwe ni uongo mtupu. Kama hiyo ni kweli, basi hawawezi kusamehewa wala kuepuka adhabu.

Nahodha, baada ya kuagiza mfanyakazi wa kike wa ngazi ya chini kutangaza kwamba abiria wanatakiwa kukaa mahali walipo, alitoroka vizuri kabla ya mtu mwingine yeyote. Inanikumbusha tukio la kihistoria wakati wa Vita vya Korea – wakati Rais Rhee Seung-man, baada ya kutangaza kwamba “sasa hali ni shwari”, walikimbia baada ya kukata daraja mto Han. Imekuwa ni zaidi ya miaka 60, lakini historia inajirudia.

Mamlaka bado haijaweza kuthibitisha nini kilichosababisha tukio hilo, na uvumi mbalimbali imeibuka, ikiwa ni pamoja na feri inaweza kuwa iligonga mwamba. Hivi sasa, wengi wanatoa lawama kwamba meli ilifanyiwa utengenezaji kinyume cha sheria[ko] ili kuwabeba abiria zaidi. Watumiaji mtandao Korea wakijadili siri ambazo hazijatatuliwa.

Kuna maswali yaliyobaki: 1) jinsi gani feri ilizama katika eneo hilo na hakuna mwamba na hali ya hewa ilikuwa nzuri siku hiyo 2) Upande wa kulia wa sehemu kuu ya Feri kumebonyea sana. 3) Tangazo la “kaeni mlipo” wakati meli ilianza kuzama4) wafanyakazi na nahodha kuokolewa kwanza 5) wito wa dhiki ulifanywa saa 8:58 na abiria 6) mvuvi mdogo kuona kuna kitu kisicho sawa na Sewol saa 7:30.

Wengi walilaumu hisia na kuchukulia urahisi kupitia kwa vyombo vya habari.

Kama ukiangalia ripoti ya awali ya gazeti la Munhwa, unaweza kuona jinsi walikuwa wavivu katika kuripoti suala hili. Mazungumzo MBC kuhusu fedha za [bima] hata kabla ya operesheni ya kuwaokoa kumalizika. KBS inalenga zaidi juu ya majibu ya rais kuliko waathirika na taarifa juu ya ujumbe wa kuwaokoa (kupitia mwanabloglu kwenye mtandao kupitia alama ashiria “Mimi ni Peter”)

Ujumbe wa kuwaokoa unaendelea. Hata hivyo, jamaa na familia ya waathirika walitoa taarifa [ko] kukemea kwamba bado hakuna taarifa zinazoeleweka pamoja na habari za kutiwa chumvi kuhusu ukubwa wa timu ya waokoaji.

도착시간 5시 30분쯤 진도 실내체육관 비상상황실에 와보니 책임을 가지고 상황을 정확히 판단해주는 관계자가 아무도 없었습니다다. 심지어 상황실도 없었습니다다.[...] 어제 현장을 방문했습니다. 인원은 200명도 안됐고, 헬기는 단 두대. 배는 군함 두척. 경비정 2척. 특수부대 보트 6대. 민간구조대원 8명이 구조작업 했습니다다. 9시 대한민국 재난본부에서는 인원 투입 555명. 헬기 121대. 배 169척으로 우리아이들을 구출하고 있다고 거짓말 했습니다.

Tulipofika saa 5:30 katika ukumbi wa michezo wa Jindo ambapo ni kituo cha dharura, hakukuwa na mfanyakazi ambaye alikuwa na wajibu wa kuwaambia watu nini kinaendelea. Hakukuwa hata na kituo cha udhibiti [...] Sisi tulitembelea eneo la ajali jana. Timu ya kuwaokoa ilikuwa chini ya watu 200 Kulikuwa na helikopta mbili tu, mashua mbili baharini, mashua mbili za walinzi wa pwani, mashua sita ya vikosi maalum.. Na watu wanane wa timu ya uokoaji wamefanya zoezi la kuokoa. Hata hivyo, Makao Makuu ya maafa yamesema uongo kwetu sisi kwamba wao waliwapeleka wanachama 555 wa uokoaji, helikopta 121 na mashua 169.

**Ripoti zaidi itafuatilia kuhusu maafa.

Gazeti la Kifaransa Lachapisha Chati Inayoonyesha Mataifa Yanayoongoza kwa Uhalifu

$
0
0

Gazeti la Le Progrès la jijini Lyon, Ufaransa ilichapisha chati [fr] yenye jina la “”Délinquance : à chacun sa spécialité – principales nationalités impliquées” (Uhalifu: Mataifa yanayohusishwa zaidi na [kila aina ya uhalifu]) (Ona picha katika mtandao wa twita hapa chini):

Katika machapisho yake ya kila siku, gazeti la Le Progres ilithubutu kuchapisha ulinganisho wa viwango vya uhalifu katika mataifa mbalimbali

Thibeau Perezat anabainisha kuwa gazeti hilo hata hivyo halikutaja vyanzo vya takwimu hizo. Mchangiaji wa Global Voices Julie Owono alisema kwamba gazeti lilishindwa kutofautisha kuwa “Waafrika” au “Roma” si mataifa.

Ni “Udhaifu” wa Serikali, Yasema Ripoti ya Ajali ya Kivuko cha Korea Kusini

$
0
0
Yellow Ribbons tied by citizens, hoping for miracles, at one random street of Seoul, Image by author.

Utepe wa njano ukiwa umefungwa katika mtaa wa Seoul kwa matarajio ya muujiza wa janga la kivuko cha Sewol. Picha na Lee Yoo Eun.

Zimetimia siku 14 tangu kivuko cha Korea Kusini kizame kikiwa na abiria mamia kadhaa. Mpaka sasa, watu wapatao 205 wamethibitishwa kupoteza maisha, na wnegine 97 bado hawajulikani walipo.

Nahodha na wafanyakazi wote wa kivuko wote wamewekwa ndani. Waziri Mkuu Chung Hong-won tayari amejiuzulu kufuatia serikali kushutumiwa kuwa ilichelewa kuchukua hatua kukabiliana na janga hilo. Watu watatu kutoka kwenye ofisi ya Incheon ya Chama cha Usafiri wa Majini cha Korea nao wamekamatwa kwa tuhuma za kuharibu ushahidi.  

Wakati taarifa zaidi kuhusu uzembe wa serikali ya Korea Kusini katika kushughulikia ajali hiyo  zimepatikana, hasira za wananchi zimeendelea kuongezeka. 

Kwenye mtandao, watumiaji wa intaneti wamezilaumu mamlaka za serikali na vyombo vya habari kwa kuendelea ‘kuimba’ visingizio vinavyotolewa na serikali: 

Mbinu mbovu za kukabiliana na majanga, udhaifu na uongo, na vyombo vya habari vinavyoendelea kudanganya mfululizo…Yote haya yameziumiza familia. Katika ajali hii ya kivuko cha Sewol, udhaifu wa serikali hii umefunuliwa.

Rais haonekani kwenye taarifa za habari. Madudu ya idara za serikali na makosa mengi na kushindwa kwa serikali havionekani kwenye taarifa za habari. Kama ilivyotokea kwenye kuzama kwa kivuko cha Sewol, nahodha wa meli alikimbia. 

Vyombo vya habari vinaonyesha video inayoonesha vifaa vilivyookolewa kutoka kwenye eneo la ajali ya kivuko hicho na vipande vya video zilizotengenezwa na wataalamu wakati wa zoezi la ukoaji. Inaonekana zoezi hilo linaendelea kwa ufanisi -kama tunategemea kupata habari kupitia vyombo vya habari pekee. Hata hivyo, hakuna wahanga wengine ukiacha wale waliokuwa wameokolewa katika eneo la ajali. Hakuna maendeleo, lakini vyombo vya habari vinaendelea kupiga porojo. Eneo hasa ilikotokea ajali ni tofauti na lile linaloonyeshwa na vyombo vya habari.

Hasira imechochewa zaidi na wanasiasa wanaoonekana kutumia tukio hilo kisiasa.

Mbunge wa chama tawala cha Saeunri yuko kikaangoni kwa kumtuhumu kimakosa mzazi wa mmoja wa wahanga wa ajali hiyo [ko] kuwa mtu asiyehusika ‘anayetaka kuchochea tu hasira dhidi ya serikali'. Mbunge huyo baadae alieleza kwamba alikuwa amepotoshwa na picha bandia zilizokuwa zinasambaa mtandaoni.  

Polizi hivi sasa wanamchunguza mwandishi  [ko] aliyeandika kwenye mtandao wa Facebook kwamba “Janga la kivuko cha Sewol ni tukio lililotengenezwa na vibaraka wa Korea Kaskazini wanaotaka kutengeneza mazingira ya hali ya sintofahamu na tahayaruki katika jamii ya Korea Kusini. “ 

Sasa mbinu za kuwaita watu “wakomusnisti wekundu” na “Vibaraka wa [Korea] Kaskazini” limekuwa jambo la kawaida siku hizi. Hali hii inaudhi sana. Kila mmoja anamtuhumu mwenzake kuwa ni “Kibaraka wa kaskazini” au “Shushushu wa Korea Kaskazini” kila panapokuwa na hali ya kutokuelewana. Watu wale ambao bado hawajakata tamaa na zoezi la uokoaji linaloendelea, watu hao ambao wako katika wakati mgumu wanaweza kuumizwa kirahisi na matamshi ya namna hiyo. Tuangalie kile tunachokisema.

Wakati nchi yote imezizima na kukata tamaa na kukaongezeka sauti za watu wanaoikosoa serikali, chama tawala na wafuasi wake wameanza kutengeneza propaganda ya “Vibaraka wa Kaskazini”. Mazingira haya yamenifanya vifikiri kuhusu kile kilichoifanya nchi yetu iingie kwenye matatizo. Kama hatuwezi kubadili uongozi unaofunika udhaifu wake kwa mbinu za eti ‘Ukibaraka wa Kaskazini', basi hatuna jawabu.

Nigeria: Kampeni ya #Bringourgirlsback

$
0
0

 


Bango la kampeni. Wasichana 234 wenye umri kati ya miaka 16-18 walitekwa nyara takribani wiki mbili zilizopita nchini Nigeria: #bringourgirlsback. Chanzo: Ukurasa wa Facebook #bringourgirlsback ‬- Kwa matumizi ya Umma

Katikati ya mwezi Aprili, zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari, iliyoko eneo la Chibok, Nigeria kitendo kinachodaiwa kufanywa na Boko Haram, kundi la kigaidi lililoko katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Ingawa baadhi ya wasichana 57 wameweza kutoroka, bado wengine wengi wako mikononi mwa watekaji nyara. Tarehe Aprili 30, wanawake wa Nigeria waliandaa maandamano katika miji kote nchini Naijeria kushurutisha serikali iongeze jitihada zake za kuwaokoa wasichana hao. Tovuti ya waandishi wa habari wa sahara walichapisha chanjo ya picha kutoka Kaduna, Nigeria. Wanablogu wa Nigeria pia walifungua ukurasa wa mtandao wa Facebook kupitia alama ashiria #bringourgirlsback, kutoa wito wa kueneza hasira zao kwenye mtandao dhidi ya hatua hii ya makosa ya jinai ya waasi wenye msimamo mkali.

Mapigano ya Wanakijiji Kugombea Ardhi Yasababisha Maafa Nchini Madagaska

$
0
0

Blogu ya L'Express Mada ilitoa taarifa kwamba kijiji kizima cha Andranondambo kilichoko Kusini mwa Madagascar kiliharibiwa [fr] kufuatia mapigano ya wanakijiji yaliyosababishwa na mzozo wa kumiliki ardhi. Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ambayo ilidumu kwa siku tatu kati ya Mei 20-22, ilipoteza maisha ya wanakijiji wote. Akikumbuka tukio hilo, mmoja wa maafisa wa polisi anasimulia [fr]:

A notre arrivée, un chien errant était en train de dévorer un bras arraché d’ un corps. Dans une maison anéantie par les flammes, nous avons mis la main sur une dépouille. L’air était irrespirable [..] Même l’école publique et l’église d’Andranondambo ont été ravagées. Les toitures en tôle ont été arrachées avec tous les mobiliers.

Tulipowasili, mbwa alikuwa akila mabaki ya maiti. Katika nyumba jirani iliyokuwa imeharibiwa kwa moto, tulikuta maiti zaidi na uvundo usiovumilika. Hata shule za umma na makanisa vyote vilikuwa zimeharibiwa. Vifaa vyote kutoka kwa nyumba vilikuwa vimetawanyika.

Mgogoro wa ardhi ulianza mwaka wa 1991 wakati madini ya mica yilipogunduliwa katika kijiji hicho cha Andranondambo. Kukimbilia kwa wachimbaji wa ardhi kulipelekea wanakijiji kuhamia mbali katika kijiji kingine cha Ambatotsivala. Tangu wakati huo, vijiji hivi viwili vimekuwa na mgogoro juu ya haki za ardhi lakini mgogoro haujawahi kufikia kiwango cha taabu ya vurugu hadi hivi karibuni.


Sisi Ashinda Uchaguzi wa Rais Misri; Mpinzani Pekee Sabahi Ashika Nafasi ya Tatu

$
0
0

Hatimaye Misri imepata rais mpya katika uchaguzi wa tatu kufanyika baada ya miaka mingi. Jenerali Abdel Fattah Al-Sisi alishinda kwa kishindo, akimbwaga mpinzani wake wa pekee Hamdeen Sabahi, ambaye amekuwa wa tatu. Baada ya siku tatu za upigaji kura, matokeo ya awali yametangazwa. Sisi ametangazwa kushinda kwa asilimia 93.3 ya kura, wakati Hamdeen akijikusanyia asilimia 3 na asilimia 3.7 zikitangazwa kuharibika.

Kwenye mtandao wa Twita, watumiaji wa mtandao wa twita walipokea habari hizo kwa kejeli na dhihaka.

Mmisri Aida Elkashef anasema [ar]:

Kinachokufanya ucheke na kulia kwa wakati ule ule ni kwamba kwenye uchaguzi huu, uliokuwa na wagombea wawili tu, Hamdeen kawa wa tatu baada ya idadi ya kura zilizotangazwa kuharibika

Sherief Gaber anauliza:

Kwa hiyo kama mwaka 2011 kulikuwa na upinzani, je tunaweza kuita uitikiaji huu mdogo kwa Sisi kuwa ni upinzani kinyume chake?

Na Mmisri Hosam El Sokkari anabainisha [ar]:

Binadamu ni mnyama wa kupiga kura (zaidi ya uwezo huo hana maana yoyote) T

Wakati huo huo, Nabeel anashangaa kwa nini watu wamekasirishwa kwa nini Sabahi hakugombea. Anauliza:

Kwa nini kumbebesha lawama Hamdeen? Kwa sababu amepata kura kidogo? Nani alidhani angeshinda?

Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Sisi, Amro Ali anaonyesha changamoto:

Sisi hataweza kuwa kama Nasser mpaka aweze kupata ushindi wa asilimia 99.9 alioupata Nasser kwenye uchaguzi wa mwaka 1956.

Mwandishi wa mtindo wa dhihaka mwenye asili ya Lebanoni Karl Sharro anaongeza:

Unaweza kusema kuwa Sisi sisi hawezi kupata zaidi ya asilimia 100 ya kura kwa sababu ya uchovu wa kimahesabu tu

Kutoka Bahrain, Abo Omar Al Shafee alifananisha matukio hayo na hali ya mambo nchini Bahrain. Anatwiti:

Kama ambavyo uchaguzi wa rais ulivyofanikiwa nchini Misri, uchaguzi wa wabunge umekuwa wa mafanikio nchini Bahrain. Hakuna faraja kwa wale waliosusia

Na, kwa kuhitimisha, mwanaharati wa Kimisri Alaa Abdel Fattah alitwiti:

Umegeuka na kuwa mjinga sana [Jenerali] Sisi

Polisi wa Masedonia Wawalazimisha Waandishi Kufuta Picha za Ghasia

$
0
0

Waandishi wa Kimasedonia walilazimishwa kwa nguvu na polisi kufuta picha na video walizokuwa wamezipiga kwenye matukio ya ghasia zilizoibuka wakati wa maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi, hali iliyosababisha kuteketezwa kwa mali kadhaa za umma  kwenye mitaa ya Gorce Petrov jijini Skopje. 

Maafisa wa polisi walianza kwa kuwakamata maandamanaji 27, ambao ni waandishi wa Radio Free UlayaNovaTV, na Focus wanasema wao pia ni shababa ya polisi kwa kuwa wanazo picha za tukio hilo. Polisi waliwasukuma na kuwaburuza waandishi, huku afisa mmoja akifikia hatua ya kuichukua kamera na kufuta kipande cha video yeye mwenyewe. 

Ghasia wakati wa nyakati zajioni za tarehe 19 na 20 mwezi Mei, 2014 zilikuwa ni  mwitikio wa mauaji ya kijana asiye na hatia mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa ndio kwanza amemaliza sekondari baada ya yeye na baba yake kumfukuza mwizi aliyekuwa ameiba baiskeli yao.

Mtuhumiwa kwa sasa aliyeko mahabusu kwa tuhuma za mauaji ni wa asili ya Albania, na wakati ghasia zikisababisha hali ya kutokuelewana kati ya watu wenye asili ya Albania na wenzao wa Kimasedonia waishio Skopje, raia wa Masedonia wenye asili tofauti walitoa mwito kupitia mitandao ya kijamii kuwaomba wananchi wenzao kuwa watulivu na kumaliza hali hiyo.

Mwanaharakati wa Kimasedonia Biljana Ginova aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba watu wote nchini humo wanaugua maradhi ya chuki. Bandiko lake kwenye mtandao wa facebook lilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na baadae kuhamia kwenye vyombo vikuu vya habari.

Треба да сме револтирани оти полицијата која ја плаќаме не нѐ штити, не е на наша страна, таа е само оружје на истите сеирџии кои од фотелјите нѐ гледаат како гинеме 

Tunapaswa kukengeuka kuwa tunawalipa polisi ili wasitulinde, hawako upande wetu na wanatumiwa tu kama silaha na watu wale wale wanaotutazama tukifa wakiwa kwenye viti vyao.

Masedonia ni makazi ya watu milioni 2.1, ambao asilimia 63 wana asili ya Masedonia na asilimia 25 ni wa asili ya Albania. Nchi hiyo ina historia ya misuguano ya kiubaguzi na kutokuvumilia, ya hivi karibuni kabisa ikiwa ni mgogoro uliotumia silaha wa mwaka 2001 kati ya vikosi vya usalama vya Masedonia na waasi wenye asili ya Albania. Hali hiyo ilimalizika kwa  Mpango wa Makubaliano wa Ohrid uliotoa haki kwa walio wachache kwa Waalibania nchini humo. 

Walio wachache waliokuwa miongoni mwa wale walioandamana kwenye mitaa yote ya jiji la Skopje, walifunga mitaa, wakitupa mawe kwa maafisa wa usalama, wakichoma majengo, na wakitoa matusi kwa watu wa asili ya Albania. Polisi waliwatupia mabomu ya machozi ili kuwatawanya, wakati wazee wanaoishi sehemu hizo waliwaomba polisi kutumia nguvu za wastani kupambana na waandamanaji wakisema, “Msiwaburuze namna hiyo!”

prevrteniKontejneriGorce20maj1

Picha ya A1on, imetumiwa kwa ruhusa.

Mwandishi kutoka kwenye chombo cha habari cha mtandaoni kiitwacho NovaTV, Sashka Cvetkovska, aliiambia Radio Free Ulaya kwamba walikuwa wamepewa ruhusa na polisi kupiga picha na kuchukua vieo za ghasia hizo, lakini mambo yanaonekana yalibadilika wakati polisi walipoanza kuwakamata waandamanaji:

Со многу висок тон и речиси насилно почнаа од нас да бараат да ги избришеме сами снимките. Една од колешките ја турнаа, мене ме влечеа за рака, не навредуваа. Јас одбив да ги избришам снимките, не ја дадов камерата, при што едниот од полицајците насилно ми ја одзема и почна самиот да брише 

Walianza kutufuata na kwa kweli ni kama walitumia nguvu kututaka tufute vyote tulivyokuwa tumevipiga kuhusiana na tukio hilo. Mwenzangu mmoja alisukumwa, mimi mwenyewe nilivutwa kwa nguvu mkononi huku nikidhalilishwa. Nilikataa kufuta nilivyokuwa nimevirekodi na sikuwapa kamera yangu, na baada ya hapo mmoja wa maafisa wa polisi aliichukua kwa nguvu na akaanza kufuta kwa mikono yake mwenyewe.

Mwandishi Meri Jordanovska wa tovuti ya Plusinfo alisema walishuhudia polisi wakitumia nguvu wakati wakimkamata kijana na kumweka chini ya ulinzi: 

Го влечеа за земја, го фатија за раце, а кога падна на земја го удрија со клоци. И ние тоа го снимавме и го фотографиравме

Walimkwida kwa mikono, wakamvuta akaanguka na wakaanza kumpiga mateke. Hayo yote tuliyarekodi kwa picha za mnato na za video..

Waandishi walifungua malalamiko kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani dhidi ya ukatili uliofanywa na polisi, lakini waligonga mwamba. Wizara hiyo ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosema:

Од извршените разговори со сите 34 полициски службеници кои учествувале во активностите на полицијата, не може да се утврди дека некој воопшто бил инволвиран во настан како што е наведен во претставката, односно одземање и бришење на снимен видео-материјал и фотографии.

Baada ya kuongea na maafisa wote 34 wa polisi walioshiriki kwenye zoezi hilo la kipolisi, hatuwezi kuthibitisha kwamba wote waliotajwa kwenye malalamiko walihusika kwenye tukio hilo, au walinyang'anywa na kufutiwa picha na video zao.

Mwakilishi wa Shirika la Usalama na Ushirikiano wa Ulaya Dunja Mijatovic alionyesha kusikitishwa mno na tabia ya polisi hao kwa waandishi waliokuw wakitafuta habari za maandamano hayo jijini Skopje:

Новинарите мора да бидат во можност да  покријат демонстрации слободно и без страв од малтретирање. Секое прекршување на правата на новинарите е јасно кршење на правото на слобода на медиумите и не може да се толерира.

Waandishi wa habari lazima waweze kuandika habari za maandamano kwa uhuru na bila wasiwasi wa kubughudhiwa. Kuvunja haki za waandishi ni wazi ni uvunjaji wa haki ya uhuru wa vyombo vya habari na hali hiyo haitavuliwa.

Umoja wa Waandishi wa Habari Nchini Masedonia vile vile ulilaani vitendo hivyo vya polisi: 

Kushinikiza kufutwa kwa picha na video kulikofanywa na polisi kunaonyesha wazi kuvunjwa kwa Ibara ya 16 ya Katiba inayozuia kufuatiliwa na inayotuhakikishia upatikanaji huru wa habari na uhuru wa kupokea na kusambaza habari. Kwa tabia hii   polisi wamewazuia waandishi kuandika/kutangaza tukio hilo na kujipa jukumu la kufuatilia na kuamua kile ambacho kinaweza kuonwa au kutokuonwa na umma wa Wamesedonia.

Kikundi cha Kitalibani Chasema Shambulio la Uwanja wa Ndege wa Karachi Lililoua Watu 24 Lilikuwa ‘Kisasi’

$
0
0
Photo tweeted by Twitter user @ahsannagi #KarachiAirport. Pic by a friend stuck there - M. Qasim. #Rangers can be seen.

Picha ilikuwa kwenye twiti ya mtumiaji wa Twita @ahsannagi #KarachiAirport. “Picha iliyotumwa na rafiki yangu aliyeko uwanjani – M. Qasim. #Wanajeshi wanaweza kuonekana kwenye Uwanja wa Ndege”

Hii ni habari inayoendelea kuandikwa. Habari za hivi karibuni ziliingia saa 12:22 GMT, Tarehe 9 Juni:

Kikundi cha kigaidi cha Tehreek-i-Taliban Pakistan (TTP)  kimedai kuhusika na tukio hilo , kikisema kuwailikuwa ni kulipiza kisasi kufuatia shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Pakistani kwenye mpaka wa nchi hiyo na Afghanistani.

Gazeti la kila siku linaloongoza la Pakistani, Dawn linasema kuwa operesheni ya kijeshi ilianzishwa upya kwenye uwanja wa ndege wa Karach, kufuatia  majibizano ya risasi, yaliyoanza masaa kadhaa baada ya jeshi kusema kwamba lilikuwa limefanikiwa kurejesha hali ya usalama kwenye uwanja huo wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi nchini humo, kufuatia uvamizi wa wanamgambo wa kigaidi kuteka uwanja huo kwa masaa sita na kupoteza maisha ya watu wapatao 24. 

Kutoka kwenye gazeti hilo la Dawn: “Tumeanza operesheni mpya na tumeita vikosi vipya,” alisema Sibtain Rizvi, msemaji wa kikosi cha jeshi cha Karachi.

Kabla ya saa 11 alfajiri, kwa saa za Pakistani, jeshi lilitoa taarifa kwamba wavamizi wote 10 walikuwa wameuawa. Wanasemekana waliingia uwanjani humo kwa kutumia vitambulisho bandia vya wanausalama wa uwanja huo wa ndege  wakiwa na , silaha kali na mabomu ya kutupa kwa mkono.

Karachi Airport employees being escorted out of Jinnah International Airport. Photo tweeted by Dawn_com

Wafanyakazi wa Uwanja wa Karachi wakisaidiwa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jinnah. Picha ilitwitiwa na @Dawn_com


Mtu mmoja alijitoa mhanga wakati wa shambulizi hilo. Watu 14 waliokuwa wafanyakazi wa uwanja huo, wengine wakiwa wafanyakazi wa shirika la ndege la taifa la Pakistani na vikosi vya usalama vile vile walipoteza maisha. Wasafiri wote waliokuwa wamekwama kwenye ndege wakati mapambano hayo yakiendelea waliokolewa na kupelekwa kwenye sehemu ya kukaa abiria baada ya shambulio hilo kumalizwa. Wanamgambo hao waliharibu ndege tatu ambazo hata hivyo hazikuwa na abiria ndani.

—————————————–

Sehemu ya zamani ya kupumzikia abiria katika uwanja wa ndege mkubwa zaidi nchini Pakistani - Uwnaja wa Ndege wa Kimataifa wa Jinnah ilikumbwa na shambulizi zito lililofanywa na wanamgambo wenye silaha usiku wa kuamkia Jumatatu. Wanamgambo wote wenye silaha wanasemekana kuingia kwenye sehemu hiyo ya uwanja iliyokuwa imetengewa kwa ajili ya watu maarufu na shughuli za ndege za Hajj, lakini kwa mujibu wa ramani ya uwanja huo, ndege zote huchangia njia moja ya kupaa au kutua.

Mtumiaji huyu wa Twita – Syed Saim Rizvi – alikuwa kwenye ndege ya Emirates iliyokuwa uwanjani humo wakati wa mapambano hayo:

Sina maneno ya kusema kwa ajili ya wafanyakazi wa Emirates, ambao wanajitahidi kuwatuliza abiria

Mlipuko wa kutisha!!! Sijui kinachoendelea mule ndani….milio ya risasi imeanza tena -humu kwenye ndege watu wako kwenye tahayaruki mno!

Awali alikuwa ametwiti:

Bado niko kwenye ndege -mfanyakazi wa emirates aliamuru mapema kwamba abiria washuke lakini kwa sasa imebidi tubaki kwenye ndege. Milipuko mikubwa inasikika

Hivi ndivyo shambulio lilivyofahamika:

Shughuli za kutua na kupaa kwa ndege zimesitishwa kwa muda kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa Jinnah ulioko Karachi kufuatia hali ya kukosekana usalama. Tafadhali piga simu namba 114 kwa taarifa zaidi.

Uwanja wa ndege wa Karachi umetekwa na washambuliaji wa kigaidi wanaosemekana kuwa kati ya 15 -20. Hali ya hatari imetangazwa katika viwanja vyote vya ndege vya Pakistani

Picha ya rafiki yangu aliyekwama ndani ya ndege. Wanajeshi wanaweza kuonekana.

Makomandoo na magaidi wanajibizana kwa risasi wakati huu. Bado ninasikia kwa karibu. Idadi ya washambuliaji inasemekana kuwa kati ya 10 -15.

Approx 4-5 hand grenades used in the attack. Dark smoke visible from where planes were. #karachi— عادل (@aurAdil) June 8, 2014

Kadri ya mabomu ya kutupwa kwa mkono yapatayo manne hadi matano yametumiwa kwenye mashambulizi. Moshi mzito inaonekana nyuma palipokuwa na ndege

Katika hali hii ya kusikitisha, maombi yangu yaende kwa familia za wafanyakazi wa uwanja huu na wa mashirika ya ndege ambao mpaka sasa wamethibitika kupoteza maisha yao kwneye uwanja huu

Lililo muhimu zaidi, bado kuna abiria waliokwama kwenye ndege iliyokuwa kwenye njia ya kutua ndege.

Magaidi watatu wako ndani ya uwanja. Milio ya milipuko inasikika. Bila shaka kila mmoja yuko salama

Wakati washambuliaji na operesheni ikiendelea baadhi ya watu waliisifu anuani ya twita ya @AirportPakistan:

@AirportPakistanni mfano wa namna mamlaka zinapaswa kutumia mitandao ya kijamii wakati wa majanga ili kutoa habari na kurekebisha tetesi na uvumi.

Habari sahihi kwa wakati muafaka kuhusu ratiba za ndege na utaratibu wa kuelekeza ndege kutua kwingineko

Baadhi ya watu walifananisha shambulio hili kwneye uwanja wa ndege wa Karachi na lile la eneo la Mehran  lililotokea Karachi mwaka 2011.

Je, ni kwamba tunashuhudia tukio jingine la #MehranBase?

Katika shambulio lililopita la Mehran ilichukua siku mbili kurejesha hali ya usalama…na hili ni kubwa mara kumi ya eneo la Mehran…!!!

Wakati vyombo vya habari vikitangaza habari za operesheni maalumu ya kijeshi, baadhi ya watu walilalimika kuhusu kutokuwepo kwa usalama kwenye eneo la uwanja wa ndege.

Shambulizi la GHQ, Shambulizi la Mehran, SHambulio la PAF, Shambulio la uwanja wa ndege wa Khi, na sasa uwanja wa ndege wa Jinnah, ndugu zangu msiogope, tuna vyombo madhubuti kabisa vya usalama kuzidi vyote duniani

Kazi za ndani ya uwanja huo kwenye sehemu ya kupakua na kupakia mizigo nayo imeshambuliwa kama ilivyokuwa Mehran. Sehemu ya kutua na kupaa kwa ndege zimedhibitiwa…vyombo vya usalama vya Pakistani viko juu

Kwa hiyo kiongozi shupavu: “Nawaz Sharif amewaelekeza wanajeshi kuhakikisha usalama wa abiria wote kwneye uwanja wa ndege

Kwa bahati mbaya, kama ilivyo kawaida ya uandishi wa habari kadri zinavyotokea, kulikuwa na tarifa za kujichanganya kuhusu idadi hasa ya washambuliaji, pamoja na tetesi kuhusu ndege kulipuliwa au kutekwa, hapa unaweza kuona baadhi ya miitikio kutoka kwneye mtandao wa Twita dhidi ya taarifa za utatanishi zilizokuwa zinatangazwa:

Mtu si awaambie watangazaji a vyombo vikuu vya habari kwamba kanuni ya kwanza ya kutangaza habari ni kutokuonyesha uko upande gani? Wanachokifanya ni dalili kwamba hawajafuzu vyema

Vyombo vya habari LAZIMA vichukue hatua ya kurudi nyuma SASA. Hakuna haja ya kutangaza mbinu za kijeshi au kutoa habari za tetesi zisizo na ushahidi

Vyombo vya kijinga vya habari vinatoa taarifa za uongo kuhusu shambulio la uwanja wa Karachi. Ndege haijatekwa. Wamezidiwa sasa na Polisi

Vyombo vya habari vinaonyesha kwa kina kila kinachoendelea wakati huu kwa matangazo ya moja kwa moja. Je, havikupaswa kuficha baadhi ya taarifa?

Hapana ndege haijatekwa wala magaidi hawajaingia kwneye ndege yoyote isiyo na aibiria

Twiti hii ilitumwa wakati wanajeshi wa Pakistani walipoungana kwneye operesheni iliyokuwa inafanywa na wanajeshi wakishirikiana na vyombo vya usalama vya uwanja huo wa ndege. Waziri Kiongozi wa Sindh pia aliwasili kwenye eneo la tukio kukagua hali ya usalama.

Waziri Kiongozi Sindh ana makomandoo zaidi kuliko waliopo kwenye uwanja wa ndege wa Khi sasa hivi? Hiki ni kioja kwa serikali ya Sindh isiyokuwa na aibu!!!

Hii ni habari inayoendelea kuandikwa kadri habari zinavyoendelea kupatikana, kwa habari za hivi karibuni zaidi fuatilia@AirportPakistan, @AsimBajwaISPR

Simulizi la Kusikitisha la Ibrahim na Djouma wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

$
0
0
Ibrahim and Amadou - screen capture of UNHCR video on YouTube

Ibrahim na Amadou – picha iliyopigwa kwenye video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia wakimbizi (UNHCR) kwneye mtandao wa YouTube

Djouma na Amadou Moussa ni wazazi wa Ibrahim. Djouma na Ibahim ni wahanga wa shambulizi la kikatili lililofanywa na  wanamgambo waaasi, tukio lililokatisha maisha ya ndugu watano wa damu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Kameruni. Wanamgambo hao walikuja wakati  Amadou Moussa akiwa mbali na nyumbani kwake. Djouma, 30, anakumbuka tukio hilo baya

Walinikuta nikiwa na wanangu nyumbani kwangu; waliwakusanya watoto wote wadogo na kuwachinja kwa panga. Waliua watu sita, ikiwa ni pamoja na watoto mbele yangu [..] Ibrahim alikuwa kati ya watoto sita waliowachukua. Walimkata na panga, wakadhani amefariki.

Kama inavyoonekana kwenye video hii, Ibrahim ana kovu kubwa kichwani kwake lililosababishwa na panga. Hata hivyo Ibrahim alipona, pamoja na tukio hilo baya. Hadithi ya Ibrahim ni mfano wa madhila ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wakimbizi 20,000 wamevuka mpaka tangu kuanza kwa vita. Ombi maalum limetumwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry kumkumbusha kuchukua “hatua stahiki za kuhakikisha  kwamba mikakati ya kurejesha amani inatengewa fedha kwa mwaka wa 2015.”

  

 

Maandamano Makubwa Yafanyika huko Guangzhou, China

$
0
0

Mamia ya wakazi wa Guangzhou jana mchana walikusanyika huko Sanyuanli kupinga hatua ya polisi ya kutaifisha mali binafsi za watu kwenye bohari kama sehemu ya harakati za kukabiliana na majanga ya moto. Waandamanaji walijikuta wakikabiliana vikali na polisi, na baadae, wakati wa vurugu hizo, waandamanaji walifikia hatua ya kupindua magari ya polisi. Charles Liu kutoka nanfang.com anayo habari kamili.

Viewing all 93 articles
Browse latest View live