Quantcast
Channel: Global Voices in Swahili » Habari za Hivi Punde
Viewing all 93 articles
Browse latest View live

Hadithi ya Wakimbizi wa Njaa kutoka Niger katika Algeria Mashariki

$
0
0

Katika wiki chache zilizopita, mamia ya wahamiaji mwa Jangwa la Sahara kutoka Mali au Niger wamehamia miji ya Algeria katika mpaka wa Mashariki. Liberté Algérie anasimulia hadithi ya wale ambao waliamua kuhama na kwa nini [fr]

Les conditions de vie au hangar de la cité Bourroh sont inhumaines. A l’intérieur du hangar, les Subsahariens ont dressé des tentes, une soixantaine environ. A l’intérieur de chaque tente, trop exiguë, vivent, serrés les uns contre les autres, tous les membres d’une même famille. [..] Meriem et Aïcha sont deux sœurs âgées respectivement de 10 et 12 ans. Avec leur mère, elles ont fui leur pays d’origine, le Niger, à cause de la pauvreté. “Nous avons quitté notre pays, parce que nous n’avions plus quoi manger. Meriem et Aïcha sont deux sœurs âgées respectivement de 10 et 12 ans. Egalement originaires du Niger, Sakina, sa fille Asma et ses deux petits-enfants s’étaient réfugiés à Aïn Guezzam, dans la wilaya de Tamanrasset, à l’extrême sud du Sahara. Dans un arabe approximatif, notre interlocutrice nous apprendra qu’ils font partie d’un groupe qui a fui la faim au Niger.

Hali ya maisha katika majengo ya mji wa Bourroh si ya kibinadamu. Ndani ya jengo, wahamiaji wa Jangwa la Sahara wameweka mahema karibu sitini. Ndani ya kila hema (ndogo sana), wao wote wanaishi pamoja, dhidi ya kila mmoja, washiriki wote wa familia moja. [..] Meriem na Aisha ni dada wawili wenye umri wa miaka 10 na 12. Na mama yao, walikimbia nchi yao ya asili, Niger, kwa sababu ya umaskini.. “Tulihama nchi yetu kwa sababu hatukuwa na chakula cha kutosha ‘Meriem anasema. Pia kutoka Niger, Sakina, binti yake Asma na wajukuu wake wawili ni wakimbizi katika Ain Guezzam katika Wilaya ya Tamanrasset, kusini mwa jangwa la Sahara. Akisita kwa lugha ya Kiarabu, Sakira alituambia kwamba wao ni sehemu ya kundi ambao walikimbia njaa kubwa nchini Niger.


Maandamano ya Kudai Haki ya Kubusu na Barua ya Haki za Mashoga Nchini Cuba

$
0
0
Foto Jorge Luis Baños, usada con permiso.

Picha imepigwa na Jorge Luis Baños, imetumiwa kwa ruhusa.

Kwenye “Maandamano ya Pili ya Kubusu au ‘Besada’ kama yanavyojulikana, kuhimiza Tofauti na Usawa” yaliyofanyika Havana, Cuba, kama “shinikizo la Mapinduzi ya Kubusu”, mabusu ambayo yanasemekana kuwa ni jitihada za kimapinduzi. Hata hivyo, tukio la pili la “Besada” linakuja wakati ambao kuna utata kuhusu kuondolewa kwa kipengeele cha kusitisha ubaguzi wa utambulisho wa kimapenzi katika sheria mpya ya Kazi nchini humo.  

Mradi wa Rainbow Project au Proyecto Arcoiris, mradi wa kupinga ubepari na mradi wa uhuru, unaratibu shughuli nzima jijini Havana, Cuba, Juni 28, Siku ambayo inafahamika kama Fahari ya Mashoga na Wasagaji, kukukumbuka Ghasia za Hoteli ya Stonewall jijini New York mwaka 1969, zilizobadili historia ya haki za mashoga na wasagaji.

Siku hiyo hiyo mwaka 2012, Arcoiris waliratibu tukio la kwanza la “Besada,” na karibu watu 50 walihudhuria tukio hilo katika maeneo ya uwanja wa michezo wa Ramon Fonst, kwenye manispaa ya Plaza Havana. Safari hii maandamano yalifanyika Plaza Vieja, jengo lililopo kwenye mji huo mkuu.

Waratibu walieleza nia hasa ya kukumbukumbu hiyo:

Besarse en el espacio público debería ser derecho de toda persona, pero para muchos ojos constituye escándalo público, si no ocurre entre heterosexuales. Al besarnos todos y todas, por amor o fraternidad, ejercitamos nuestra igualdad ciudadana y ponemos en evidencia los dobles raseros morales que generan la homofobia, el sexismo, las lógicas discriminatorias que marcan las raíces de nuestra cultura y debemos cambiar.

Kupigana busu hadharani lazima iwe haki ya kila mmoja, lakini wengi wanaona harakati hizo kama kashfa ya wazi wazi, hasa kama inatokea kati ya watu wa jinsia moja. Kama wanaume na wanawake wanapobusiana, iwe kwa mapenzi au kwa kufahamiana, wanafanya hivyo kututumia haki yao ya usawa kama raia na inakuwa ni kuonyesha ajabu kuona kuwa kufanya hivyo ni kukuza hisia woga na chuki kwa mashoga, hali za kimapenzi, na hisia za kibaguzi zinazokuwa mzizi wa utamaduni wetu na ambazo lazima tuzibadilishe.

Zaidi ya kuchapishwa kwenye blogu ya Arcoiris, ujumbe ulisambazwa kwenye tovuti kadhaa za intaneti, moja wapo ikiwa Cubainformacion.tv. Zaidi, majarida kadhaa yanayochapishwa kwenye kisiwa hivyo, kama La Jiribilla na Cuba Contemporánea, zimeandiska kuhusu tukio hilo.

Barua ya kuzindua tukio hilo inaongeza: 

Porque Revolución es cambiar todo lo que deba ser cambiado, y defendemos la idea de una sociedad anticapitalista, revolucionaria y democrática. Ven y celebra que la Ley No.116 Código de Trabajo protege por primera vez a las personas homosexuales. Ven y reclama explicación pública a la eliminación de la identidad de género y el estatus frente al VIH en la misma Ley, aunque la Asamblea Nacional lo aprobó.

En esta cita no importan el color de la piel, el género, la identidad de género, las creencias religiosas o políticas, la orientación sexual, el origen territorial, la discapacidad ni cualquier otra distinción, sino la fe en la igualdad de todas las formas de amar, formar familia, producir, comprometerse… todas las formas de HACER PATRIA.

28 de junio, pon la Revolución en un Beso.

Kwa sababu mapinduzi yanamaanisha kubadilisha kila kitu kinachopaswa kubadilihswa, na tunatetea wazo la kupingana na ubepari, tunatetea jamii ya kimapinduzi na kidemokrasia. Ungana nasi na sherehekea Sheria ya kazi No 116, ambayo kwa mara ya kwanza inalinda haki za mashoga. Njoo uombe maelezo ya kina tena kwa uwazi kuhusu kuondolewa kwa masuala ya utambulisho wa kijinsia na hali ya afya kuhusiana na maambukizi ya UKIMWI katika sheria hiyo, ingawa Bunge la Taifa halijaipitisha bado.

Siku hiyo, rangi ya ngozi yako, jinsia, utambulisho wa kijinsia, itikadi za kidini na kisiasa, hali ya kimapenzi, asili ya utaifa, ulemavu natofauti nyinginezo hazitakuwa na maana yoyote, maana kile tunachofanya ni imani katika usawa wa namna zote za mapenzi, utengenezaji wa familia, kuzaliana, kujitoa…namna zote ya KUWA WAZALENDO.

Siku ya Juni 28, leta Mapinduzi katika Kubusu

Mukhtadha ambao tukio la “Besada” linafanyika ni utekelezaji wa Sheria Mpya ya Kazi, iliyoondoa mapendekezo ya  Mariela Castro Espín, mbunge wa Bunge la Cuba na shushushu maarufu wa nchi hiyo, kwamba utambulisho wa kijinsia una nia ya kuwabagua watu kwenye mazingira ya kazi. 

Waandishi kadhaa na wanablogu wameonyesha kutokuridhika na matokeo ya Sheria mpya ya Kazi, ambayo ilitoka kwenye kujadiliwa mpaka kuchapishwa kwenye Gazeti rasmi la Serikali ya Cuba liitwalo Gaceta Oficial de la República de Cuba bila kupitishwa kwa mabadiliko ya mwisho. Castro Espín alijadili suala hili kwenye tovuti yaKituo cha Taifa cha Elimu ya Jinsia(Centro Nacional de Educación Sexual ‘Cenesex'), taasisi anayoingoza.

Wanachama wa Mradi wa Arcoiris walituma barua kwa Esteban Lazo Hernández, mwenyeketi wa Bunge la Taifa la nchi hiyo. Hapa chini tunakupatia waraka huo kamili:

La Habana, 23 de junio de 2014

Año 56 de la Revolución

A: Esteban Lazo Hernández

Presidente de la Asamblea Nacional del Poder Popular

Compañero:

La Gaceta Oficial de la República de Cuba acaba de publicar el texto definitivo de la Ley No.116 Código de Trabajo, y quisiéramos esclarecernos sobre los motivos de la ausencia en esta norma jurídica de elementos que muchas personas esperábamos hallar, luego de la discusión y aprobación de esta ley por nuestro máximo órgano legislativo, el cual usted preside.

Todo nuestro pueblo pudo ver por la Televisión Cubana el debate que sobre esta legislación aconteció en el Parlamento durante sus sesiones ordinarias de diciembre de 2013. Aquel análisis incluyó varias propuestas de la diputada Mariela Castro Espín, quien fue portavoz de un grupo de planteamientos hechos por trabajadores y activistas como parte del amplio proceso de consulta popular del anteproyecto de Ley.

Entre esas sugerencias estaba la inclusión de la identidad de género y el estatus frente al VIH como motivos por los cuales no resulta admisible discriminar a ningún ser humano en el ámbito laboral, dentro de los principios fundamentales que rigen el derecho al trabajo, en el inciso B del artículo 2 de ese cuerpo legal.

Miongoni mwa mapendekezo lilikuwa suala la kuingizwa kwa utambulisho wa kijinsia na hali ya afya kuhusiana na virusi vya Ukimwi kama

Sin embargo, a pesar del apoyo a esos pronunciamientos por otras diputadas y diputados, y de la intervención del primer vicepresidente cubano Miguel Díaz-Canel, quien abogó por tener en cuenta lo allí dicho y encargar esa encomienda a una comisión parlamentaria, esos dos aspectos no aparecen en la ley ahora publicada.

El asunto nos alarma no solamente porque ello implica un presunto desconocimiento de la voluntad expresa de varios integrantes de la Asamblea Nacional del Poder Popular, así como por lo grave que esto pudiera ser en relación con los principios y procedimientos democráticos que debieran regir el funcionamiento del Parlamento.

Pero incluso nos preocupa más la trascendencia humana y política de estas adiciones que fueron ignoradas sin explicación aparente, pues son las personas con una identidad de género trans las que más discriminación social y laboral sufren en nuestro país, y tampoco es un problema del todo resuelto el estigma y los prejuicios hacia las personas con VIH/sida, también en cuanto a sus capacidades profesionales y el derecho que les asiste a ejercer en cualquier tipo de empleo.

Por tanto, como ciudadanos y ciudadanas de este país, y también en nuestra condición de activistas por los derechos humanos y sexuales que defendemos la idea de una sociedad anticapitalista, revolucionaria y democrática, solicitamos una explicación pública sobre los criterios que siguió la mencionada comisión parlamentaria para excluir de la versión final de la Ley No.116 las citadas propuestas de modificación al proyecto de Código de Trabajo.

Agradecemos de antemano cualquier gestión que usted pueda realizar para responder con la mayor agilidad y total transparencia a nuestra respetuosa y cívica petición.

Saludos cordiales,

Integrantes de Proyecto Arcoíris. Colectivo LGBT, anticapitalista e independiente de Cuba.

Correo: proyectoarcoiriscuba@gmail.com. Blog: http://proyectoarcoiris.cubava.cu/

                                                                                                                                                       

Havana, Terehe 23 Juni, 2014

Mwaka wa 56 wa Mapinduzi

Kwenda kwa: Esteban Lazo Hernández

Mwenyekiti wa Bunge la Taifa la Serikali ya Watu

Ndugu:

Hivi karibuni, Gazeti la Serikali ya Cuba lilichapisha kwa kina maudhui ya Sheria ya ya kazi Na 116, na tungependa kuwa wazi kuhusu sababu za kutokuwepo kwa masuala kadhaa ambayo watu wengi wanegtamani kuyaona kwenye sheria hiyo, baada ya kujadiliwa na kupitishwa kwa sheria, na chombo cha juu kabisa chenye maamuzi ya kisheria, ambacho wewe ni kiongozi.

Mji wetu wote ulitazama, kwenye televisheni ya Cuba, mjadala wa sheria hiyo ulivyokuwa unaendelea Bungeni wakati wa mikutano yake ya kawaida mwezi Desemba 2013. Uchambuzi huo mahususi ulifuatiwa na mapandekezo kadhaa kutoka kwa Mbunge Mariela Castro Espín, ambaye ni msemaji anayekutana na wafanyakazi na wanaharaki kama sehemu ya mchakato wa wazi wa ushauri wa kiutaalamu wa muswada wa sheria.

Miongoni mwa mapendekeo hayo kulikuwa na kipengele cha kuweka utambulisho wa kijinsia na hali ya afya ya Ukimwi kama sababu ambayo haikubaliki kwa binadamu kubaguliwa katika mazingira ya kazi, haki inayoangukia kwenye kanuni za msingi zinazoongoza haki za kazi, kwenye sehemu B, Ibara ya 2 ya waraka huo wakisheria.

Hata hivyo, pamoja na msaada wa matamko haya kutoka kwa Wabunge, na hatua ya makamu wa rais wa Cuba Miguel Díaz kuingilia kati, aliyetetea msimamo uliowekwa na Tume ya Bunge, mambo hayo mawili bado hayaonekani kwenye muswada wa sheria hiyo.

Suala hili linatustua, si kwa sababu tu lina maana ya kutokufahamu yaliyosemwa na baadhi ya wabunge wa Bunge la Taifa, pamoja na unyeti wa suala lenyewe linapokuja suala la misingi ya kidemokrasia na hatua linazopasa kufuatwa katika utendaji bora wa Bunge.

Kinachotupa wasiwasi ni umuhimu wa binadamu na siasa ambao tunaupuuza bila maelezo yanayoeleweka. Watu wenye kupenda mapenzi ya jinsia moja ndio ambao wamekuwa wakihusika na masuala mengi ya kijamii na ubaguz wa kikazi katika nchi yetu, na wala hatujawahi kuona unyanyapaa na hisia za ubaguzi kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi zikipatiwa majibu yake kikamilifu, na pia kuhusu uwezo wao wa kitaalam na haki ya kutafuta aina yoyote ya kazi.

Henceforth, kama raia wa nchi hii, na pia kama watu na wanaharakati wa haki za kimapenzi wanasimamia wazo la kupinga ubepari na kupigania jamii ya kimapinduzi na kidemokrasia , tunaomba maelezo kuhusu kigezo ambacho tayari kimetajwa na tume ya bunge ikifuatiwa na amri ya kutoa, kwenye toleo ya Sheria Na 11, pendekezo la kurekebisha muswada wa Sheria ya Kazi.

Tunatanguliza shukrani kwa jitihada zako katika kujibu maombi haya ya heshima na kiraia mapema na kwa uwazi unatakiwa.

Wako mtiifu,

Wanachama wa Proyecto Arcoiris. Umoja wa Mashoga na Wasagaji, Wapinga ubepari na watetezi wa Cuba.

Barua pepe: proyectoarcoiriscuba@gmail.com. Blogu: http://proyectoarcoiris.cubava.cu/

 

 

Ni Rasmi Sasa, ‘Shoga’ wa Kwanza Kuteuliwa Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Nchini Puerto Rico

$
0
0
Maite Oronoz durante el proceso de confirmación en el Senado de Puerto Rico. Imagen tomada de video.

Maite Oronoz wakati wa zoezi la kuthibitishwa kwenye baraza la seneti la Puerto Rico. Picha imepigwa kwenye video iliyowekwa na Baraza la Seneti.

[Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa za lugha ya Kihispania, isipokuwa ikionyeshwa vinginevyo.]

Mnamo Jumatatu, Juni 23, 2014, Baraza la Seneti la Puerto Rico lilimthibitisha mwanasheria Maite Oronoz Rodríguez [en] kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo. Uteuzi huo wa kihistoria unakuwa wa kwanza kwa mtu aliyejitangaza kuwa msagaji kuteuliwa kuitumikia mahakama kuu kabisa nchini humo. Oronoz Rodríguez, ambaye anakuwa mwanamke wa tano kuitumikia Mahakama Kuu, alitoa shukrani zake kupitia tamko la maandishi [en]:

Ninayo furaha kwamba mchakato wa kidemokrasia umesababisha niteuliwe. Ninajivunia kuendelea kuitumikia nchi yangu, wakati huu kwenye Mahakama Kuu. Kujitolea kwangu kwa nchi yangu na kwa katiba ya Puerto Rico kutaendelea kuwa imara. Kupitia kwangu, watu wa Puerto Rico watapata jaji mwaminifu wa mtenda haki, mtiifu kwa katiba ya nchi. Ninamshukuru Gavana na Baraza la Seneta kwa fursa ya kuthibitisha kujitolea kwangu.

Kura ya kumthibitisha Oronoz Rodríguez ilikabiliwa na upinzani mkali, kura 16 zikimkubali na 10 zikimkataa [Oronoz aliteuliwa na gavana wa Puerto Rico, Alejandro García Padilla, wa chama cha Kidemokrasia cha Partido Popular Democrático]. Katika kura zilizomkataa Oronoz Rodríguez ilikuwemo ya Seneta pekee wa kike, wa chama cha Puerto Rican Independence Party, María de Lourdes Santiago. Santiago alieleza kuwa uamuzi wake ulizingatia uhusika wa Oronoz Rodríguez katika kashfa za siku za nyuma, ambapo inadaiwa akiwa mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Manispaa ya San Juan alitetea uamuzi wa Meya wa kuruhusu kukaguliwa kwa kila mtu ambaye angehudhuria Sherehe za Mtaa wa San Sebastian. Kukaguliwa kulithibitishwa na mahakama ya sheria kuwa kinyume na katiba.

Mchakato wa kuthibitishwa haukupia hivi hivi. Baada ya kura iliyomthibitisha Oronoz Rodríguez kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, baadhi ya maseneta waliomba kuhesabiwa upya kwa kura. Amárilis Pagán (@AmarilisPagan), mwanasheria wa kutetea haki za Mashoga (LGBT), alionyesha kusikitishwa kwake na mchakato huo:

Kama pasingekuwa na hofu na chuki dhidi ya mashoga mjini humu, tusingekuwa na zengwe hili la kuthibitishwa kwa Oronoz. Ni mchosho wa taifa. 

Mwanaharakati wa Haki za Mashoga Pedro Julio Serrano alikisifu kitendo cha Oronoz Rodríguez wakati wa mchakato wa kuthibitishwa: 

Maite se presentó sin miedo – con todas sus identidades a flor de piel y ante la vista del País. Su nombramiento merecía esa misma valentía. Lo tuvo, a final de cuentas, pero de manera atropellada. Hay que ir de frente, sin miedo, de cara al sol, con respeto y dignidad. Como merecemos las personas LGBTT, como merecemos tod@s l@s seres human@s.

Maite alijieleza bila hofu – akijitambulisha kikamilifu kama mpenda nchi. Uteuzi wake [kama Jaji] unathibitisha hili. Ilitokea, mwisho wa siku, lakini kwa namna ya kushangaza. Lazima tuendelee mbele, bila woga, tukilitazama jua, kwa heshima na hadhi inayostahili. Kama watu wapendao mapenzi ya jinsia moja wanavyostahili. Kama binadamu wote wanavyostahili.

Jaji mpya alipongezwa na wabunge wa nchi hiyo, Luis Gutiérrez na Nydia Velázquez kupitia mtandao wa twita:

Ni siku kubwa kwa usawa wa kimapenzi na haki kwa mashoga. Ninampongeza gavana kwa kumteua Maite Oronoz Rodriguez kuwa jaji

Si tu kuwa Maite Oronoz atakuwa jaji bora lakini uteuzi wake kuwa jaji wa Mahakama Kuu ni hatua moja mbele kwa haki za kiraia

Katika safu ya jarida la mtandaoni 80 grados, mwanaharakati Yoryie Irizarry (@CyborgYoryie) alilitazama tukio hili la kihistoria kama matunda ya mapambano ya muda mrefu ya kudai usawa yaliyoongozwa na jumuiya ya mashoga na wasagaji:

A diferencia de lo que piensan nuestras aliadas y aliados, yo he decidido pensar que ese momento histórico no nos viene cortesía del gobernador Alejandro García Padilla. Este momento histórico nos lo hemos ganado en las calles, en las legislaturas, en nuestras comunidades y empleos, educando, haciéndonos visibles, deponiendo, escribiendo, firmando cartas, debatiendo y trabajando.

Kinyume na kile washirika wetu wanavyodhani, nimeamua kufikiri kwamba tukio hili la kihistoria halijatokea kwa nguvu za Gavana Alejandro García Padilla. Tumeshuhudia tukio hili mitaani, bungeni, na kwenye jamii zetu na kwenye shemu zetu za kazi, kuelimisha, kujitangaza, kushuhudia, kuandika, kusaini barua, kupambana na tunaona kazi inaendelea.

Mjadala wa umma ulionzishwa na uteuzi wa Oronoz Rodríguez unabainisha mwamko endelevu wa hali ya kimapenzi hata kwa watu maarufu, kufikia mahali masuala ya msingi, kama uwezo na uelewa wake, vitafutika kwa sababu tu ya hali yake ya kimapenzi. Katika makala yake kwa jarida la mtandaoni la El Post Antillano, Jaime Pieras Castañer alielezea tatizo hilo:

Cuando se discutía el nombramiento en los medios se enfatizaba demasiado en la orientación social de la nominada. Aparentemente, hubiese estado bien si no fuese sincera sobre su orientación sexual, pero lo dijo. Thomas Rivera Schatz, ex presidente del Senado, expresó en un apasionado discurso [...] en el Senado que ella era la que había traído a la atención que era lesbiana. Bah, como si eso tuviese que ver con sus clasificaciones o con las consideraciones que deben de ser parte de cualquier deliberación sobre los dotes o el talento de Oronoz.

Vyombo vya habari vimeupa uteuzi huu sura ya mwelekeo wa kijinsia wa mtauliwa. Kwa hakika, ingekuwa vyema kama asingekuwa wazi kuhusu hali yake ya kimapenzi, lakini ndio hivyo, alishajitangaza. Thomas Rivera Schatz, rais wa zamani wa Seneti, alisema kwenye hotuba yake kali [...] kwneye Seneta kwamba [Oronoz Rodríguez] mwenyewe ndiye aliyelileta suala la usagaji wake hadharani. Utafikiri hali yake ya kimapenzi ina maana yoyote kwa sifa zake au iwe sababu yoyote ambayo yapaswa kuwa sehemu ya mjadala wa vipaji na uwezo wa Oronoz.

Érika Fontánez Torres, mwanasheria, Profesa wa Sheria na mhariri wa jarida la mtandaoni Derecho al Derecho, anatoa maoni ya kusisimua kwenye podikasti ya jarida hilo (kwenye dakika ya 11:20):

Hay alguna gente que a raíz de toda esta discusión ha dicho “no, es que no es importante, no es relevante que ella sea lesbiana o no” y, bueno, lo primero que tendríamos que decir, “sí, que sí que lo es”, […] sí que las subjetividades son importantes en el Tribunal, sí que añaden a la mesa, sí que la diversidad es importante a la hora de la deliberación de los jueces […], y si esa persona tiene, como en el caso de Maite Oronoz, una experiencia de vida desde esa ubicación, eso me parece extraordinario.

Kuna baadhi ya watu waliojibu mjadala huu kwa kusema, “Hapana, si tatizo, haina maana awe ni msagaji au sio,” lakini sawa, jambo la kwanza tunalopaswa kuwa tunalisema ni “Ndio, ndo, ni muhimu”…ndio, maamuzi binafsi ni muhimu kwenye mahakama, ndio, yanaleta jambo fulani kwenye kazi zake za kila siku, ndio, tofauti ni muhimu majaji wnaapotekeleza kazi zao [...], na kama mtu binafsi, kama Maite Oronoz, ana uzoefu wa kimaisha kwa mtazamo huo, ningeweza kusema kwamba kuwa hilo ni suala kubwa isivyo kawaida.

Wamalaysia kwenye Ndege MH17 Iliyoanguka: “Bila Kujali Utaifa, Tuko Pamoja Kuomboleza””

$
0
0
Family members rushed to Kuala Lumpur International Airport when informed about the flight MH17 crash. Photo by Danny Chan, Copyright @Demotix. (7/18/2014)

Wanafamilia wakikimbilia uwanja wa ndege wa kimataifa Kuala Lumpur baada ya kujulishwa kuwa ndege MH17 imeanguka. Picha na Danny Chan, Haki miliki @Demotix. (7/18/2014)

Ndege ya Malaysia ya MH17, iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kwenda Kuala Lumpur, imeanguka mashariki mwa Ukraine jioni ya Alhamisi, ikiwaua abiria  298 pamoja na wafanyakazi waliokuwepo ndani.

Taarifa nyingi zinaonyesha kwamba ndege hiyo ilitunguliwa na silaha umbali wa kilimeta 50 kutoka kwenye mpaka wa Urusi na Ukraine. Serikali y Ukraine inawatuhumu wapinzani wanaoungwa mkono na Urusi kutumia silaha kali kuitungua ndege hiyo lakini viongozi wa waasi wanakana madai hayo.

Picha ya mchoro inaonesha njia ya ndege hiyo na eneo ilikoangukia ndege ya MH17:

Picha ya mchoro: Ramani ikionesha eneo ilikoanguka ndege ikiw ni pamoja na njia ya ndege MH17

Waziri Mkuu wa Malaysia Najib Razak aliwahakikishia wananchi wake kwamba wale waliohusika kuitungua ndege hiyo watapelekwa kwenye mkono wa sheria:

Leo ni siku mbaya, katika mwaka ambao tayari ni mbaya, kwa Malaysia.

Kama itajulikana kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kwa hakika, tunasisitiza kwamba waliohusika wanakabiliana na mkono wa sheria.

Abiria wa ndege hiyo na wafanyakazi walitoka katika nchi mbalimbali.

Lakini leo, bila kujali uraia, wote tuko pamoja kuomboleza.

Alifafanua kwamba njia ya ndege hiyo angani, hata kama ilikuwa inapita juu ya eneo lenye mgogoro, ilitangazwa kuwa salama na Shirika la Kimataifa la Safari za Anga.

Flight MH17 crashed in eastern Ukraine. Photo by  Danny Chan, Copyright @Demotix (7/18/2014)

Ndege MH17 ilianguka mashariki mwa Ukraine. Picha na Danny Chan, Haki Miliki @Demotix (7/18/2014)

Kuanguka kwa ndege MH17 kumekuja katika kipindi kifupi ambacho bado dunia inakumbuka kupotea kwa Ndege ya shirika la Malaysia Boeing 777-200 mwaka huu. Mnamo Machi 8, ndege ya Malaysia MH370 iliyokuwa na watu 237 ndani yake ilipotea saa moja tu baada ya kupaa kwenye uwanja wa Kuala Lumpur wakati ikisafiri kuelekea Beijing. Ndege ya MH370 na abiria wake bado  hawajulikani walipo.

Binti wa mfanyakazi wa ndege hiyo MH370 alitwiti kuwafariji ndugu na marafiki wa abiria wa ndege ya MH17:

Nikiwa mwanafamilia wa mfanyakazi wa ndege MH370, na kwa niaba ya wote, ninawaombea abiria wa ndege MH17. Muwe na moyo mkuu rafiki zangu.

Josie Fernandez wa shirika la Kimataifa la Uwazi Malaysia alitoa wito wa uchunguzi wa kina wa ajali hiyo:

Kilichotokea hakikubaliki – Malaysia ni nchi pekee ambapo shirika hilo hilo, aina hiyo hiyo ya ndege zimehusika kwenye majanga yanayopoteza maisha ya watu wengi ndani miezi michache. Ndege MH370 haijapatikana.

Malaysia lazima iombe kuchukuliwa kwa hatua za Kimataifa kwa janga hili lisilokubalika. Ndege hii ilikuwa ya abiria. Hatuko vitani na taifa lolote.

Akiandikia gazeti la The Ant Daily, Alyaa Alhadjri alilieleza tukio hilo la kutunguliwa kwa ndege ya MH17 kama ‘mauaji ya halaiki’:

Kwa nini abiria wa ndege ya kibiashara waruhusiwe kupita kwenye eneo lenye mgogoro ambapo ndege zimekuwa zikitunguliwa na walitahadharishwa kusafisha anga.

Kwa sababu yoyote iliyosababisha kuanguka kwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia Boeing 777 kwa mara ya pili ndani ya siku, na kupoteza watu 537 katika majanga mawili ya anga, haisaidii kuinua imani ya wasafiri kwa shirika hilo la ndege.

Wakati Malaysia ikiomboleza kufuatia ajali nyingine ya ndege, inaonekana kuwa raia wengi wataendelea kuishinikiza serikali kueleza hali hiyo ya ‘sintofahamu’ iliyosababisha kupotea kwa kwa ndege MH370.

Matamshi Matano ya Kushangaza Kufuatia Kuanguka kwa Ndege MH17 Nchini Ukraine

$
0
0
So much for "knowing that feel," when it comes to polemics surrounding the downed Malaysian airliner. Images mixed by Kevin Rothrock.

Kuna namna nyingi “kujua mtu anavyojisikia,” ukifuatilia matamshi yanayotolewa baada ya kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia. Picha zimechanganywa na Kevin Rothrock.

Maafisa, wanasiasa na waandishi maarufu wa Kirusi walikuwa wepesi kutoa maoni kuhusiana na ajali ya Ndege ya Malaysia MH17, iliyoanguka Mashariki mwa Ukraine siku ya Alhamisi, Julai 17. Mamlaka za Kyiv, Moscow, na Donetsk zimekuwa zikishutumiana, kubebeshana lawama kwa kutunguliwa kwa ndege hiyo ya abiria na kuua watu wote karibu 300 waliokuwemo ndani yake. Wakati hisia zikiendelea kuongezeka, matamko machache yaliyotolewa na watu mashuhuri mjini Moscow na Donetsk yamevutia hisia ya watumiaji wa Intaneti mtandaoni. 

1. Katika hili, hatukufanya.

Waziri Mkuu aliyejitangaza mwenyewe wa Jamhuri ya watu wa Donetsk, Aleksandr Boroday, hakuwa na uhakika kuhusiana na uhusika wa waasi katika tukio hili:

Bahati mbaya, hii ni nukuu ya siku. [Maneno yanasomeka, "Kama ni kweli ni ndege ya abiria, basi haikuwa sisi," Alexandr Boroday.]

2. Ina maana yoyote kujua nani alifanya kitendo hiki?

Leonid Kalashnikov, naibu mwakilishi wa kamati ya Bunge la Urusi ya mambo ya kimataifa, aliiambia TV Rain haikuwa na maana yoyote kujua nani wa kumlaumu kwa kuiangusha ndege hiyo:

“Вам что, легче станет, если узнаете, кто сбил самолет?”

“Nini, utajisikia nafuu kaa utamjua aliyeiangusha ndege hiyo?”

3. Uovu wa hali ya juu

Akiwa ameumizwa na kile waasi wa Urusi na ‘waendesha propaganda’ wa Ukraine walichokirudia mara kwa mara hisia zile zile (kwamba walikosoa serza ya Urusi kwa Ukraine), Konstantin Rykov wa chama tawala cha siasa Urusi alikuwa na haya ya kusema:

Katika nyakati kama hizi ni wazi kuna watu wanatarajia kitu na wanacho wanachokitaka…wapigania uhuru wetu na wapiga propaganda wa Ukraine wanashindania kile kile…

4. Ni rahisi: hakuna wa kumlaumu

Mkuu wa shirika la Russia TodayMargarita Simonyan alionyesha namna janga hilo lilivyo na faida kwa wa-Soviet wasio na akili:

Kw amuda mrefu nimekuwa nikifanyia kazi taarifa kadhaa za habari zinazotokea, na nimehitimisha kuwa siamini kabisa namna watu wanavyojaribu kuunganisha matukio kujengea hoja imani zao. Lkaini ninaamini kuwa Usoviet ina matatizo. 

5. Waasi? Waasi gani?

Mwisho lakini si kwa uzito ni mwitikio wa Vladimir Putin mwenyewe, aliyeliambia shirika la habari la ITAR-TASS kwamba Kyiv inawajibika kwa anga la Ukraine mashariki inayodhibitiwa na waasi.

“Безусловно, государство, над территорией которого это произошло, несет ответственность за эту страшную трагедию. [...] Этой трагедии не произошло бы, если бы на этой земле был мир, не были бы возобновлены боевые действия на юго-востоке Украины”

“Kwa hakika, nchi ambayo mpaka wake ndiko tukio hili limetokea inawajibika kwa janga hili [...] Janga hili lisingetokea kama pangekuwa na amani kwenye nchi hiyo, kama mapigano yasingeibuka tena Kusini Mashariki mwa Ukraine.”

Je, Ujumbe wa Shirika la Ndege la Singapore Baada ya Ndege MH17 Kuanguka Haukuwa wa Kiugwana??

$
0
0
A Singapore Airlines flight on March 29, 2014. Photo by Flickr user Aero Icarus. CC BY-NC-SA 2.0

Ndege ya Shirika la Ndege la Singapore Machi 29, 2014. Picha na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Aero Icarus. CC BY-NC-SA 2.0

Baada ya habari kufahamika kwamba ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17 imeanguka mashariki mwa Ukraine, Shirika la Ndege la Singapore liliweka ujumbe huu kwenye mtandao wa Facebook na Twita:

Wateja wanaweza kuendelea kufahamu kuwa ndege za Shirika la Ndege la Singapore hazitumii anga la Ukraine

Watumiaji wengi wa mtandao walililaumu shirika hilo la ndege kwa kutokuwa na uungwana. Sophie Chang alitoa maoni kwenye mtandao wa Facebook kwamba “namna nzuri kwa shirika la ndege kufanya ni kutoa pole kwanza.” Lakini Stephen Chapman anaamini kwamba kauli hiyo “ilikusudia kuleta utulivu kwa maana pana.” Ryan Ik alikubaliana na ufafanuzi huo lakini alijisikia “kukosa maneno ya kutoa pole, habari hizo hazikuwa za kiungwana.”

Iwe ni kweli ama la kwamba ujumbe huo ulikosa uungwana, lakini tangu uwekwe mtandaoni umekuwa ukisambaa kwa kasi ndani ya masaa machache.

Israel Yaanza Operesheni ya Ardhini Gaza

$
0
0
Israel begins ground operations on Gaza. iFalasteen shares this photograph from Gaza on Twitter

Israel imeanza operesheni ya ardhini Gaza. iFalasteen anatuma picha hii kutoka Gaza kwenye mtandao wa Twita

Vikosi vya kijeshi vya Israeli vimeanza kuingia Gaza, baada ya siku 10 za mapigano zilizochukua maisha ya Wapalestina 200. M-Israeli mmoja aliuawa kwa shambulio la roketi kwenye eneo la Palestina. Hatua hiyo inakuja baada ya Hamas, kikundi kinachoitawala Gaza, kukataa pendekezo la kumaliza mapigano lililotolewa na Misri.

Tovah Lazaroff, mwandishi wa Boston aliye katikati ya mgogoro wa Israel na Palestina, anatwiti:

Ni rasmi sasa kutoka kwenye ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, vikosi vya jeshi vimeanza kuingia Gaza

Anaongeza:

Ofisi ya Waziri Mkuu: Baraza la Mawaziri limeidhinisha operesheni ya ardhini baada ua Israeli kukubaliana na pendekezo la Misri la kusitisha mapigano. Hamas ilikataa mapendekezo hayo

Ardhini huko Gaza, iFalasteen anasema:

Mabomu kila mahali hapa Gaza, hakuna umeme na kuna mwanga mkali wa milipuko na mabomu…

Mabomu yanapigwa mfululizo na hakuna pa kukimbilia…Mungu tu atailinda Gaza

Mvua ya Moto Inanyesha Gaza: Israeli Yaanza Shambulio la Ardhini

$
0
0

Wa-Palestina wanasema mvua ya moto inanyesha Gaza, baada ya Israeli kuanza operesheni ya ardhini ndani ya eneo inalolizunguka, Gaza. Gaza, inayoelezwa kama gereza la wazi, ndiko wanakoishi wa-Palestina milioni 2, ambao hawana pa kukimbilia. Israeli inapakana na Gaza upande mmoj, na Misri inaifungia kwenye upande mwingine.

Kwenye mtandao wa Twita, Jehan Alfarra, mwenye wafuasi 8,000 anasema:

Gaza usiku huu inakabiliana na uvaizi wa ardhini unaofanywa na Israeli!

Mtumiaji mwingine aitwaye Gaza Writes Back, mwenye wafuasi 36,400 kwenye mtandao wa Twita, anasema kuanza kwa uvamizi wa ardhini na milipuko mizito ya mabomu imeifanya “Gaza yote kuwa mithili ya mpira wa moto”:

Israeli imeanza uvamizi wa ardhini na kuugeuza ukanda wote wa Gaza kuwa mithili ya mpira wa moto

Na iFalasteen, vile vile akitokea Gaza, alitwiti kwa wafuasi wake 26,800:

Mvua ya mabomu inanyesha kwenye ukanda wa Gaza sasa hivi kutoka baharini, ardhini na hewani…Israeli inapiga mabomu pande zote

Pia mtumiaji mwingine akiwa Gaza, Palestine, anatuma picha hii ya milipuko ya mabomu ukanda wa Gaza usiku huu kwa wafuasi wake 10,000 kwenye mtandao wa Twita:

Ni shambulio zito linaendelea sasa!!

Kwenye picha nyingine, anasema:

Hata mwezi umekuwa mwekundu hapa Gaza usiku wa leo

Mpiga picha Jehad Saftawi anatuma picha kutoka kwenye mpaka wa Gaza, ikionyesha kuanza kwa operesheni hiyo:

Shambulio la ardhini linalofanywa na Israeli limeanza kwenye ukanda wa Gaza, hapa kwenye mpaka wa Gaza

Wakati Lara Abu Ramadan, mwandishi wa habari wa ki-Palestina, mfasiri na mpiga picha wa kujitegemea anayeishi Gaza, anaeleza:

Hali inatisha. Naweza kuona moto mkubwa kutoka kwenye matanki ya Israeli magharibi mwa ukanda wa Gaza

Na mwanablogu wa ki-Palestina Haitham Sabbah, anatoa kiungo hiki cha habari a moja kwa moja kutoka Gaza:

Habari za moja kwa moja kuhusu shambulio linaloendelea Gaza #GazaUnderAttack http://t.co/jg2PZQbXXK — Haitham Sabbah (@sabbah)

Wakati huo huo, mwandishi wa habari Richard Hall, anayeishi Paris, anawakumbusha wafuasi wake 6,000:

Mara ya mwisho Israeli kuivamia Gaza, wa-Palestina 1,387 waliuawa. 773 walikuwa wananchi wasio wanajeshi, wakiwemo watoto 320 na wanawake 109 (Chanzo: B'Tselem)

Leo ni siku ya 11 tangu kuanza kwa “Operesheni ya Kujilinda”, ambayo imepoteza maisha ya wa-Palestina 230, wakiwemo wanawake na watoto, na zaidi ya watu 1,500 wakijeruhiwa.

Kutoka Gaza, Hamas, ambayo imeutawala ukanda huo tangu mwaka 2007, ililipua makombora kwenda Israeli. Roketi nyingi zinazoingia Israeli hazijasababisha madhara makubwa, kwa sababu, kwa kiasi fulani, ya mfumo wa anga wa ulinzi unaofadhiliwa na Marekani, ambao umezuia makombora yapatayo 70 mpaka sasa, kwa mujibu wa gazeti la the Guardian.

Kwa operesheni hii ya kimakundi, madhara yanaweza kuongezeka zaidi.


Televisheni ya Taifa Urusi Yahariri Wikipedia Kuibebesha Ukraine Lawama kwa Kuanguka MH17

$
0
0
The war in Ukraine moves to Wikipedia. Images mixed by author.

Vita nchini Ukraine imeahamia kwenye kamusi elezo ya Wikipedia. Picha zimechanganywa na Mwandishi wa makala.

Siku moja baada ya tukio baya la kutunguliwa kwa ndege mashariki mwa Ukraine iliyopoteza maisha ya watu wapatao 300, maneno ya kutafuta kujua nani wa kumlaumu kwa kuitungua ndege hiyo zimepamba moto. Viongozi wa Ukraine, Urusi, na hata waasi wanaotaka kujitenga wa Donetsk wote wamekuwa wakibebeshana lawama. Jijini Kyiv, Rais Poroshenko aliwalaumu waasi mashariki mwa nchi hiyo na kuishambulia Urusi kwa kufanya hali ya mpaka iwe tete. Jijini Moscow, Vladimir Putin aliibebesha lawama Kyiv kwa chochote kinachotokea Ukraine. Kiongozi wa waasi wa Donetsk alikana kuhusika na shambulio la ndege hiyo ya Malaysia MH17, akidai limefanywa na jeshi la anga la Ukraine.

Katika hali isiyoshangaza, mchezo huo wa kulaumiana sasa umehamia kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo vita ya wahariri kuweka kumbukumbu vinazoelekeana na upande wao. Mapema asubuhi hii, ukurasa wa Kirusi wa Wikipedia ulikuwa na andiko lililohusu kuanguka kwa ndege hiyo, ambapo mtumiaji mmoja mwenye alama ya utambulisho wa kompyuta iliyoko Kyiv alihariri habari za MH17 kusema kwamba ndege hiyo ilitunguliwa ‘na magaidi waliojitangazia nchi inayoitwa Jamhuri ya Watu wa Donetsk kwa kutumia makombora ya kisasa, yaliyotoka kwenye shirikisho la Urusi.” Ndani ya muda mfupi usiozidi saa moja, mtu mwingine mwenye alama ya utambulisho wa kompyuta ya Moscow alibadili maelezo hayo na kuandika, “ndege hiyo ilitunguliwa na wanajeshi wa Ukraine.”

Shukrani kwa mtandao wa Twita unaonukuu uhariri wowote unaofanywa kwenye kamusi elezo ya Wikipedia unaofanywa na alama za utambulisho wa kompyuta zinazotumiwa na serikali ya Urusi, kwani sasa tunafahamu kuwa uhariri huo wa pili kwa makala hiyo ya MH17 ulitoka kwenye kompyuta iliyoko kwenyeKituo cha Televisheni la Taifa la Urusi.

Makala ya Wikipedia kuhusu kuanguka kwa ndege ya MH17 ilihaririwa na VGTRK.

VGTRK ambayo ni makzi ya Dmitri Kiselyov, anayefahamanika kwa jina la utani mkuu wa propaganda wa Kremlin. Kiselyov anajulikana zaidi kwa kukosoa vikali serikali za Kyiv na Washington. Wakati wa mgogoro wa Crimea, Kiselyov aliwahi kujitapa kwenye televisheni kwamba “Urusi ndiyo nchi pekee duniani iliyobaki inayoweza kuigeuza Marekani kuwa vumbi kwa mabomu ya nyuklia.” Mwezi Juni, waandishi wawili wa VGTRK waliuawa karibu na Luhansk baada ya kuunguzwa kwa moto wakiwa na waasi wa maeneo hayo. Nadiya Savchenko, rubani wa helkopta ambaye waasi walimkamata nchini Ukraine na kumsafirisha kwenye Voronezh mapema mwezi huu, sasa anashikiliwa kwenye mahabusu ya Urusi, akituhumiwa kushiriki mashambulizi yalisababisha kuuawa kwa waandishi wa VGTRK.

Akaunti ya Twita iliyogundua matumizi ya mtandao wa intaneti yaliyofanywa na VGTRK, @RuGovEdits, imetengenezwa na zana (bot) nyingine, @CongressEdits, ambayo hufuatilia uhariri unaofanywa na Wikipedia kutoka kwenye kompyuta za Bunge la Marekani. Alama maalum ya CongressEdits, ilitengenezwa na mtaalam wa program za kompyuta Ed Summers, na ni zana huria inayoweza kurekebishwa kirahisi ili kuwezesha kufuatilia utambulisho wowote wa kompyuta.

Wanablogu wa Zone 9 Washitakiwa kwa Ugaidi Nchini Ethiopia

$
0
0
Zone 9 bloggers Zelalem Kibret, Edom Kasaye, and Befeqadu Hailu. Photos used with permission.

Wanablogu wa Zone 9 Zelalem Kibret, Edom Kasaye, na Befeqadu Hailu. Picha zimetumiwa kwa ruhusa.

Wanablogu na waandishi tisa, wanne wakiwa wanachama wa Global Voices, wamefunguliwa mashitaka ya ugaidi na shughuli zinazohusiana na ugaidi mbele ya Mahakama Kuu ya Lideta nchini Ethiopia hapo jana. Wakiwa wamekamatwa na kuwekwa ndani jijini Addis Ababa tarehe 25 na 26 Aprili, wamekuwa mahabusu kwa tuhuma zisizo rasmi za “kufanya kazi na mashirika ya kigeni yanayodai kuendesha harakati za haki za binadamu na …kupokea fedha kwa ajili ya kuchochea ghasia kwa kutumia mitandao ya kijamii.” 

 Wanasheria na ndugu wa washitakiwa hao hawakupewa taarifa ya kusomewa mashitaka yao, na hivyo hakupata msaada wa kusheria wakati mashitaka yao yanasomwa.. 

Blogu ya Kufuatilia Shauri la Zone9, inayoendeshwa na watu walio karibu na washitakiwa hao, iliripoti kwamba mashitaka yao ni pamoja na kufanya kazi na mashirika yaliyopewa jina la ‘magaidi’ na serikali ya Ethiopia; kushiriki kwenye mafunzo ya kuandika barua pepe kwa lugha ya siril na “kuwa na mipango ya siri.” 

Mwanasheria wa wanablogu hao aliliambia shirika la habari la AFP kwamba mashitaka hayo “hayana maaana yoyote.” Watu wanaowaunga mkono duniani kote walionyesha hasira yao dhidi ya mashitaka hayo kwenye mtandao wa Twita, kwa kutumia alama habari ya #FreeZone9Bloggers. Yoseph Mulugeta, mwakilishi wa zamani wa shirika la Kutetea Haki za Binadamu [Human Rights Watch] nchini Ethiopia ana anayefuatilia kwa karibu kesi hiyo, alitwiti:

Mashitaka hayo ya kutunga yaliyoorodheshwa kwenye kurasa 19 hayajataja jina la Zone9 kwa jina. Hata mara moja. Jina hilo kwa hakika linawaogofya sana maadui wa uhuru wa habari

Ikiwa imetungwa mwaka 2009, sheria tata ya kupinga ugaidi nchini Ethiopia kwa bahati mbaya haifahamiki sana kwa waandishi wa habari za kisiasa nchini humo. Waandishi Eskinder Nega na Reeyot Alemu walikabiliwa na mashitaka yanayofanana na hayo na wamekuwa wakishikiliwa kwenye mahabusu ya Kalaity jijini Addis Ababa tangu mwaka 2011. Waendesha mashitaka wanasemekana kuandaa mashitaka hayo kufuatia tuhuma kwamba wanablogu hayo wamekuwa wakipokea mafunzo na misaada ya kifedha kutoka kwenye vikundi viwili vya kisiasa vyenye asili ya vilivyoko Ulaya na Marekani. Blogu ya kufuatilia shauri hilo inabainisha kwamba vikundi hivyo vinafanana kiitikadi.. 

Kwa mujibu wa taarifa mpya za habari, wanablogu na waandishi hao wanatuhumiwa kujiunga kinyume na sheria kama muungano wa wanablogu wa Zone9, shitaka la ajabu, kwa kuzingatia mwonekano wa wazi wa blogu ya Zone9 na shughuli zinazoendeshwa na kikundi hicho.

Kesi ya kundi hilo itasikilizwa tena Agosti 8. Tembelea Blogu ya Kufuatilia Mwenendo wa Mashitaka hayog kwa taarifa zinazojitokeza kuhusu kesi hiyo na kuona namna unavyoweza kuwaunga mkono wanablogu hao wa Zone9.

Free Zone9 Bloggers campaign image. Created by Hugh D'Andrade, remixed by Hisham Almiraat.

Picha ya kampeni ya kuwatetea wanablogu wa Zone9. Imetengenezwa na Hugh D'Andrade, na kuchanganywa na Hisham Almiraat.

Miezi Michache Baada ya Kupotea kwa MH370, Kuanguka kwa Ndege Nchini Ukraine Kwawashitua Raia wa Malasia

$
0
0
A relative of those on board flight MH17 getting emotional while being interviewed by media. Photo by Hon Keong Soo. Copyright @Demotix (7/18/2014)

Ndugu wa baadhi ya watu waliokuwa wakisafiri kwa ndege aina ya MH17 akionesha uso wa huzuni pale alipohojiwa na vyombo vya habari. Picha na Keong Soo. Haki miliki na @Demotix (7/18/2014)

Kutokana na tukio la kuanguka kwa ndege aina ya MH17 ya shirika la ndege la Malaysia, huko mashariki mwa Ukraine, salamu za rambirambi zimekuwa zikitumwa kwa familia za abiria 298 pamoja na wafanyakazi waliokuwemo kwenye ndege hiyo. 

MH17 ilitunguliwa kwa kombora la BUK ikitokea Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur. Taarifa mbalimbali zinawahusisha waasi walio na uhusiano wa karibu na serikali ya Urusi ambao kwa bahati mbaya waliishambulia ndege ya abiria, hata hivyo, kiongozi wa waasi hao amekanusha taarifa hizi. 

Hili ni tukio la pili kuzikumba ndege za Malaysia katika kipindi cha miezi kadhaa. Ndege aina ya MH370 Malaysia iliyokuwa na watu 239 pamoja na wahudumu mnamo Machi 8 ilitoweka na haijulikani ilipo mpaka sasa.

Wakishtushwa na matukio hay mawili, raia wa mtandaoni wa Malaysia wanatumia kiungo habari cha Twita #PrayForMH17 kujadili kuhusiana na tukio hili la kuanguka kwa ndege.  

Mhudumu wa ndege ya shirika la ndege la Malaysia alijadili kwa uchache kuhusiana na idadi kubwa ya watu kupoteza maisha kwenye ndege hiyo aina ya MH17 pamoja na ile yaMH370, kwa kuweka picha katika ukurasa wa Twita na Instagram: 

Kwa kipindi cha miezi 4 nimepoteza marafiki wanaofikia 30…. inasikitisha lakini ukweli ni kuwa tunaishi katika ulimwengu uligubikwa na uadui

Image shared from a Malaysia Airlines flight attendant's Instagram

Picha iliyowekwa na mhudumu wa shirika la ndege la Malaysia Instagram

Wanasiasa wengi walitumia kurasa zao za Twita wakionesha namna walivyoguswa na tukio hili na pia kutoa maoni yao kuhusiana na kipi kifanyike kufuatia tukio hili.

Waziri mkuu, Najib Razak alitoa pole kwa familia za wafiwa:

Ninawaombea abiria na wahudumu wote wa MH17, pamoja na familia za wafiwa. Huu ni wakati mgumu sana kwetu sote.

Hishammuddin Hussein, ambaye ni waziri wa ulinzi wa Malaysia alitwiti kuhusiana na mikakati ya serikali ya Malasia: 

Mikakati yetu ya sasa ni kutaka kujua- 1) Ndege ile ilingushwa? na kama ndivyo, 2) Iliangushwaje? 3) Na nani? Vikosi vyetu vyote vya usalama wa taifa tayari vimeanza kazi.

Waziri wa Malaysia wa wizara ya Vijana na Michezo, Khairy Jamaluddin, alisisitiza kuwa lawama zisielekezwe kwa ndege za Malaysia kupita katika anga la ukanda ulio na mgogoro:  

Tunapaswa kupinga maelezo ya kulalamikia uchaguzi wa uelekeo. UHALISIA: Ndege nyingine nyingi zimepita pia katika anga hilo. UHALISIA: ICAO ilihakiki uelekeo huo.

Raia kadhaa maarufu wa Malaysia walitoa salamu salamu zao za pole na kuonesha namna walivyoguswa na tukio hili kupitia kurasa zao za Twita. Miongoni mwao ni mchezaji wa mchezo wa mpira wa vinyoya wa Malasia, Lee Chong Wei: 

Moyo wangu unasononeka sana ninaposhuhudia ndugu na wapendwa wetu waliokuwa wakisafiri na #MH17 waliopoteza maisha katika tukio hili baya na la kusikitisha.

Mtangazaji wa Televisheni na Redio, Xandria Ooi alidokeza kuwa lawama hazitasaidia kujua chanzo: 

Kusikiliza kupitia kwenye kompyuta ilisikitisha sana. Wengi wanafahamu kuwa ndege hii iliruka katika uelekeo ilipopatia ajali kwa makosa. Hili ni janga. Lawama hazisaidii.

Pang Khee Teik, mratibu wa Seksualiti Merdeka (Tamasha la usawa wa jinsia la Malasia), alituma salamu zake za pole:

Katika ulimwengu wa kusadikika, matukio ya kusadikika yanaweza kuwa na maana. Katika ulimwengu wa kusadikika, upendo wa kusadikika ndio wokovu wangu wa pekee. Ninawapenda nyote.

Kumekuwa na njama zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na kuanguka huku kwa ndege, lakini kwa jamii kubwa ya watu wa Malasia, huu ni wakati wa kuomboleza vifo vya watu wasio na hatia na kuwafariji wale wote waliofiwa.

Picha za Mabaki ya Ndege ya Shirika la Algeria AH5017 Nchini Mali Yaonyesha Ghasia, Kuanguka kwa Ghafla

$
0
0

PICHA ZA KWANZA za ndege ya AH5017 ya Shirika la Ndege la Algeria ikianguka, kupitia @AirLiveNet

Kipande cha kwanza cha video cha ajali ya ndege sasa kinapatikana. Tunamshukuru mwanajeshi wa Burkina Faso aliyekuwa eneo la tukio la ajali karibu na Gossi, Mashariki mwa Mali. Hakuna mtu aliyeokoka katika abiria 118 waliokuwa kwenye ndege hiyo, ikiwa ni pamoja na raia 50 wa Ufaransa. Tovuti la Aljeria Algérie Focus imeripoti kwa Kifaransa kwamba:

Cette vidéo montre des débris éparpillés et broyés. La zone sablonneuse a été noircie par le crash. Sur cette vidéo, il est pratiquement impossible de repérer les pièces maîtresses de l’avion au milieu des débris.

Video inaonyesha vipande vya ndege hiyo vikiwa vimetawanyika. Udongo wa eneo hilo uligeuka kuwa mweusi. Katika video hiyo, si rahisi kutambua sehemu yoyote ya ndege hiyo kwenye mabaki hayo.

Alama ya Utambulisho wa Kompyuta ya Serikali ya Urusi Yakamatwa Ikihariri Makala ya Wikipedia ya Ndege ya MH17

$
0
0

Alama kadhaa za utambulisho wa kompyuta (IP address) ndani ya serikali ya Urusi zimeendelea kufanya kazi kazi kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo kompyuta ya Shirika la Upelelezi la Urusi, FSO, ilihariri makala ya Kijerumani kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17, ikibadili neno “wanaotaka kujitenga” kuwa “waasi.” Teknolojia ya Twita ya @RuGovEdits, ambayo bila kuongozwa kufuatilia uhariri wowote unaofanywa kwenye kurasa za Wikipedia kupitia alama za utambulisho wa kompyuta za serikali ya Urusi, ilibaini majaribio saba tofauti yaliyofanywa na kompyuta za “mashushushu” wa FSO asubuhi hii kuhakikisha kuwa neno “waasi” linabaki kwenye kumbukumbu. JItihada hizo zilikwama. Wahariri wa Kamusi Elezo ya Wikipedia kwa Kijerumani walirudisha maandishi ya awali yaliyokuwepo kwenye makala hiyo, kila mara.

Uhariri wa Kamusi elezo ya Wikipedia Kijerumani kuhusu MH17 kama unavyoletwa kwako na serikali ya Urusi.

Viewing all 93 articles
Browse latest View live